Sunday, November 4, 2012

HII NDIO NIMEKUTANA NAYO LEO.



STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO TAR 5 NOV, NDIO HIZI.

HII NI NYINGINE TANESCO



Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limeenndelea kuwapanguaa wafanyakazi wake katika ngazi tofauti tofauti na kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.
Uongozi wa juu wa Tanesco unasema hadi sasa wafanyakazi 190 wa Tanesco wameshakabidhiwa barua za kuhamishwa na nusu ya watumishi hao ni katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wafanyakazi 95 wamepanguliwa kutoka katika mikoa ya Tanesco iliyopo katika Jiji la Dar es Salaam pekee na wamehamishiwa mikoani ambako wanatakiwa wawe wameripoti katika vituo vyao vipya vya kazi ifikapo Novemba 15, mwaka huu.

Kadhalika idadi kama hiyo ya watumishi kutoka mikoani wamehamishiwa Dar es Salaam, hatua ambayo inalenga kuimarisha utendaji katika jiji hilo ambalo licha ya kuwa kitovu cha uchumi wa nchi, huduma za Tanesco zimekuwa zikilalamikiwa kuwa haziridhishi.

Hatua hiyo ya kupangua wafanyakazi hasa wa Dar es Salaam, imekuja siku chache tangu Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco ilipomwachisha kazi rasmi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, William Mhando kutokana na ukiukwaji wa maadili ya uongozi.

Kadhalika tayari Tanesco imeshawafukuza kazi wafanyakazi wake 29 waliothibitika kufanya makosa ya wizi wa fedha za shirika na hujuma katika miundombinu ya umeme, huku wafanyakazi wengine 19 wakiwa wamesimamishwa kazi wakati uchunguzi wa tuhuma zao ukiwa bado unaendelea.

Wafanyakazi waliosimamishwa ni tofauti na vigogo waliosimamishwa pamoja na Mhando ambao pia hatima yao inaweza kujulikana wiki hii, baada ya uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kukamilika.

Hao ni pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Ununuzi, Harun Mattambo.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchem Mramba akizungumza na gazeti hili, alikiri kuwapo kwa uhamisho wa wafanyakazi hao na kwamba huo ni utaratibu wa kawaida wa shirika.

“Ni kweli kwamba tunafanya marekebisho ya utendaji wetu wa ndani, ni suala la kawaida tu, kwani kuna ajabu gani kuwahamisha watu? Tunaimarisha utendaji wetu, kwa hiyo mimi sidhani kama hilo ni jambo kubwa,” alisema Mramba na kuongeza:

“Nadhani ninyi mnafahamu kwamba tuna changamoto ya kukabiliana na malalamiko ya wateja wetu, tunatakiwa kutoa huduma kukidhi mahitaji yao, kwa hiyo tunajitizama hapa na pale, ili kuona kama tunaweza kuimarisha utendaji na kukidhi matakwa ya tunaowapa huduma.”

Sababu za kupanguliwa
Habari kutoka ndani ya Tanesco zinasema kuwa sababu kubwa za kupanguliwa kwa wafanyakazi hao, wengi wakiwa ni wasimamizi wa ndani na nje (supervisors & foremen), ni kuvunja mtandao wa wizi na hujuma hasa katika Jiji la Dar es Salaam.

“Watu wengine wamekaa kwenye vituo kwa miaka mitano mpaka saba, wamejenga mitandao mikubwa ya wizi wa umeme na ndiyo maana kwenye operesheni zimefanyika mmeona jinsi watu ambavyo wamekuwa wakiiba umeme,” alisema mmoja wa watumishi wa Tanesco ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe na kuongeza:

“Kwa hiyo kwa hatua hii, mtandao wa wizi na hujuma kwenye shirika ni kama umevunjwa maana nasikia kwamba uhamisho kwa ngazi za juu zaidi nao unafuata na lengo ni hilohilo”.

Mtumishi mwingine ambaye pia aliomba jina lake lihifadhiwe alisema, Tanesco huenda ikawa imepata hasara kubwa ya kifedha kutokana na wizi wa umeme ambao umekuwa ukifanywa na maofisa wa shirika hilo kwa kusadia wateja kuchezea mita, hivyo kupata umeme bure.

“Hata wale jamaa waliokutwa wakiuza kadi za Luku kule Mwananyamala, hawawezi kufanya hivyo bila kusaidiwa na wafanyakazi wa ndani ya shirika. Hivyo wapo watu waliobambwa, hao wamefukuzwa lakini wengine ambao tuhuma zao hazikuthibitishwa wamehamishwa,” alisema mtumishi huyo.

Habari zaidi zinasema wizi wa umeme ndani ya Tanesco umekuwa ukifanywa kupitia mtandao wa wafanyakazi wa idara tofauti ambazo hufanya kazi kwa kutegemeana, hivyo siyo rahisi kwa mtu mmoja kufanikisha wizi huo.

“Wizi wa hapa ni kwa mtandao, kwa mfano mtu wa hapa Kinondoni hawezi kufanikisha wizi wa units za umeme bila kushirikiana na watu wa makao makuu, nao lazima wawe wawili au zaidi, halafu hata yeye wa hapa hawezi kuwa peke yake, kwa hiyo huu ni mtandao mkubwa sana,” kilisema chanzo chetu.

Uchunguzi zaidi wa gazeti hili umebaini kwamba baadhi ya watumishi katika vituo vya Dar es Salaam ni kama wameshushwa vyeo, kwani wamehamishwa kutoka vituo vikubwa kama makao makuu ya mikoa na kupelekwa katika vituo vidogo, ambako hakuna majukumu makubwa kama waliyokuwa nayo mwanzo.

Kadhalika habari zaidi zinasema uhamisho huo, pia unawagusa watumishi walioguswa na tuhuma zaidi ya 175 zilizowasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi wakati wa kikao cha uongozi wa wizara na wafanyakazi wa Tanesco kilichofanyika Mei 19 mwaka huu.

Mramba akizungumzia tuhuma hizo jana alisema: “Hatujazikalia kimya, tuhuma hizo, tumezifanyia kazi na tuko katika hatua mbalimbali kulingana na makosa yaliyotajwa.”

Mramba katika maelezo yake alisema kati ya watumishi 29 waliofukuzwa au kuachishwa kazi na wale ambao wamesimamishwa kwa ajili ya kuchuguzwa, baadhi yao ni wale waliotajwa katika mkutano wa wafanyakazi na viongozi wa wizara.

Habari zaidi zinasema katika maeneo ambako kulikuwa na tuhuma za upotevu wa fedha, Tanesco walilazimika kufanya ukaguzi wa hesabu na kwamba katika sehemu ambako wizi au upotevu wa fedha ulithibitika, wahusika wamefukuzwa au kuachishwa kazi.

Mkutano wa Mei
Katika mkutano wa Mei, wafanyakazi wa Tanesco walimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo majina ya vigogo wa wizara yake wanaodaiwa kulihujumu shirika hilo.

Tukio hilo lilitokea wakati waziri huyo akiwa na Manaibu Waziri wake, George Simbachawene na Steven Masele pamoja na Maswi, walipozungumza na wafanyakazi wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Agizo la kukusanya majina hayo lilitolewa na Maswi muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya Shirika hilo, Abdul Mkama kutoa taarifa kwa niaba ya wafanyakazi iliyoeleza kuwa kuna vigogo katika wizara hiyo na wafanyakazi wengine wa Tanesco, wanaojihusisha na vitendo vya hujuma.

Katika mkutano huo, Mkama alisema Kamati yake ya Majadiliano inawafahamu kwa majina vigogo wa wizara  hiyo wanaojihusisha na njama za kulihujumu shirika hilo kwa lengo la kuingiza wawekezaji wanaowataka katika sekta hiyo.

Miezi miwili baada ya tuhuma hizo, Bodi ya Tanesco ilimsimamisha Mhando pamoja na watendaji wakuu wengine wa Tanesco ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Nafasi ya Mhando imechukuliwa na Mramba ambaye alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Masoko na Usambazaji wa Tanesco.

KIDATO CHA PILI LEO KIKAANGONI.

EA BREAKFAST: Mitihani ya Kidato cha Pili inaanza leo nchini Tanzania huku serikali ikisema mwisho wa kurudia mitihani ya kidato hicho ni mara moja tu na baada ya hapo mwanafunzi atatimuliwa...nini maoni yako?Wakati wanafunzi wa kidato  cha pili wananza mtihni wao wa Taifa leo hii,
Waziri wa elimu Ndg. Shukuru Kaambwa ametangaza rasmikupunguzwa kwa miaka ya kukariri darasa kwa watakaokuwa
 wameshindwa kufanya vizuri kutoka miaka mitaka mitatu hadi mwaka mmojo.

PICHA ZA MISS TANZANIA 2012 ZIKO HAPA.

 
BRIGITTE ALFRED

HII NI CHANGAMOTO NYINGINE KATIKA ELIMU.

WATANZANIA NI WATU WA AJABU SAANA, HUCHANGIA MAMILIONI YA PESA KWA AJILI YA HARUSI NA SHEREHE ZISIZO NA TIJA.
LAKINI WATANZANIA NI WAGUMU KUCHANGIA SHUGHURI ZA MAENDELEO TENA ZENYE MANUFAA..
TUBADIRIKE, TWAWEZA NI SISI....

ARUSHA KUUNDA MTEGO WA FUMANIZI, VIGOGO KUFUMANIWA

UTAPELI wa aina yake, umeibuka mkoani Kilimanjaro ambapo kundi la matapeli hula njama na wanawake kuandaa mitego ya fumanizi na kujipatia mamilioni ya shilingi.
Uchunguzi wa kina wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa kundi hilo limekuwa likiwalenga wanaume walio katika ndoa na wenye uwezo wa kifedha, ambao baada ya kunaswa katika fumanizi hizo hupigwa picha zinazogeuzwa mradi.
Utapeli huo unawalenga wafanyabiashara, watu wenye nyadhifa kwenye taasisi na hata viongozi wa dini.
Kundi hilo lenye mtandao mpana nchini, linaonekana katika siku za karibuni kujikita katika mkoa wa Kilimanjaro.
Uchunguzi huo unaonyesha kuwa katika kipindi cha wiki mbili, watu wanne wamejikuta wakinaswa katika mtego huo na kutoa kitita cha kati ya Sh3 milioni na Sh10 milioni, gharama hizo zikiwa nje ya zile za kukomboa picha.
Kundi hilo hufanya kazi kwa kuwatumia wasichana wadogo na wakubwa, ambao wanaajiriwa maalumu kwa kazi hiyo ambayo haitofautiani na ya uchangudoa.
Mbali na waume za watu, wengine ambao wamenaswa kwenye mtego huo ni  baadhi ya mapadri wa Kanisa Katoliki, ambao hulazimika ‘kumalizana’ nao wakihofia kuchafuliwa kwa kashfa iwapo jambo hilo litaanikwa kwa umma.
Katika tukio la hivi karibuni, mfanyabiashara mmoja wa mjini Moshi alinaswa katika fumanizi hilo na mwanamke mmoja aliyedaiwa ni mkazi wa eneo la KDC Barabara Kuu ya Moshi-Himo na kulipa Sh3 milioni.
“Kwa hofu ya taarifa kumfikia mkewe, jamaa yangu aliamua kutoa fedha walizotaka, na unajua unapofumaniwa akili zinapotea kwa muda na unakuwa huna ujanja,” kilidokeza chanzo chetu.
Hata hivyo, chanzo hicho kilidai kuwa baada ya kupita wiki moja, mfanyabiashara huyo alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mwandishi wa gazeti moja la udaku akimtaarifu kuwa ana picha za mfanyabiashara huyo alizopigwa kwenye fumanizi.                                                                                                                                                                                                                                                                                                          
“Baada ya hapo tuliifuatilia namba yake na tumegundua anaitwa (jina tunalo), lakini kule kwenye lile gazeti hawamfahamu kabisa wala hiyo namba hawaijui,” alidai ndugu wa mfanyabiashara huyo.
Alidai kuwa, baada ya kumfuatilia mwanamke anayedaiwa kufumaniwa na ndugu yao, waligundua pia kwamba, tukio hilo ulikuwa ni mchezo mchafu.
Ndugu huyo alidai kuwa, mwanamke huyo anafahamika mjini Moshi na kwamba, anaishi kwa ujanja-ujanja kwani hana kazi maalumu na wala hajaolewa.
Kati ya matukio 10 yaliyotokea, tapeli huyo anayejifanya mwandishi wa gazeti hilo la udaku, ndiye anayetajwa kuhusika kupiga simu, akitishia kuwa asipolipwa, atachapisha picha za fumanizi.
Imedaiwa kuwa, vigogo wenye nyadhifa mbalimbali katika taasisi kadhaa mkoani Kilimanjaro wameingia kwenye mtego huo.
Padri mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa, pia anadaiwa kunaswa katika mtego huo na kulipa Sh5 milioni, lakini baadaye alilazimika kutoa kitita kingine cha Sh3 milioni ili kukomboa picha zake.
Uchunguzi umebaini kuwa padri mwingine wa shirika moja alilazimika kutoa Sh6 milioni, baada ya ‘mwandishi’ huyo kumpigia simu akimweleza ana picha za mtoto aliyezaa na mwanamke mmoja.
“Unajua hawa wenzetu hawaruhusiwi kufanya tendo la ndoa, lakini baadhi yao tunaowafahamu wana watoto, hivyo wanapotokewa huwa wanachanganyikiwa,” alidokeza ndugu wa karibu wa padri huyo.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake waliohojiwa na gazeti hili walidai kuwa wako tayari kukilipa kikundi hicho ili waume zao wafumaniwe na kuaibishwa kama njia ya kuwarejesha kwenye mstari.
Pamoja na kukiri kuwapo kwa mchezo huo mkoani humo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema uhalifu huo ni vigumu kuudhibiti kwa vile wanaofanyiwa hivyo hawawezi kutoa taarifa polisi wakihofia wake zao kubaini uchafu wao.
Alisema kuwa,  badala ya waathirika wa matukio hayo kuwafichua wahusika wa matukio hayo, huamua kufa na tai shingoni huku wakiendelea kugeuzwa mradi na matapeli hao na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kikundi hicho cha matapeli kiweze kukamatwa.
Chanzo: gazeti la mwananchi.

MAMBO YA LIGI KUU TANZANIA BARA.

Yanga waendelea kupeta hadi kuongoza ligi kuu Tanzania bara baada ya kuichapa Azam magoli mawili nunge huku timu ya Simba nayo ikiendelea kufanya vibaya katika michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha magoli mawili kutoka kwa Mtibwa Sukari ya mjini Morogoro.
Mpaka sasa Simba wako nafasi ya pili wakifutiwa na Azam katika nafasi ya tatu.





Zilizosomwa zaidi