Thursday, November 1, 2012

HAYA NDIO MANENO YA WAZEE KUHUSU ZIWA NYASA.

WAKATI nchi ya Malawi ikiendelea kushikilia msimamo wake, kuwa mpaka Mashariki mwa Ziwa Nyasa kati yake na Tanzania unatenganishwa na ardhi ya Tanzania, Wazee wilayani Kyela, wametoboa siri na kuweka hadharani ukweli wake.
Wazee wengi waliotoa ushahidi juu ya ukweli wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi ndani ya Ziwa nyasa,  mbele Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe  walisema Malawi inasababisha chokochoko isiyo na msiongi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mstaafu, John Mwakipesile(70), ambaye alikuwa wa kwanza, kuzungumzia suala hilo, alisema anashangazwa na madai hayo mapya  ya Malawi kuwa Ziwa lote  ni  miliki yao.
Alisema kitendo hicho cha nchi hiyo kukurupuka kinapaswa kupuuzwa kwa kuwa  jambo hilo halina ukweli na linapingana na historia na desturi za kweli za maisha ya kawaida ya wananchi wa mpakani wa mataifa haya toka enzi za ukoloni.
Alisema madai ya Malawi hayajazingatia historia ya kweli ya ziwa hilo kwani madai yao  yote ni kujaribu kuficha ukweli kwa kuwa  yeye  kama kizazi cha tatu hata siku moja hakuwahi kusikia kuwa ziwa lote ni mali ya nchi hiyo.
Alisema kuna ushahidi wa kutosha juu ya Tanzania kuwa miongoni mwa wamiliki wa ziwa hilo, kwani kuna mali  za Watanzania yakiwamo makaburi ndani ya ziwa hilo baada ya kumezwa.
Alitolea mfano shule ya msingi  aliyosoma katika  mwaka 1945  kuwa ilishamezwa na ziwa hilo, yakiwemo majengo ya baraza (Mahakama) katika kijiji alichozaliwa cha Mwaya katika wilayani humo.
“Mimi kwa umri wangu wa miaka 70 ni kizazi cha tatu katika wilaya hii nakumbuka shule niliyosoma mwaka 1945 pale Mwaya nilipozaliwa ilishamezwa na Ziwa na ni umbali wa kilomita mbili toka pwani ya sasa kijijini hapo” alifafanua Mwakipesile.
Naye Maini Mwakisambwe (83), Mkazi wa Kata ya Katumba songwe, alisema tangu azaliwe alikuwa akijua mpaka  ni Mto Songwe ambao unaingiza maji ndani ya ziwa hilo  na ndio uliotumika kama mpaka wa kuligawa ziwa kwa mataifa haya mawili.
Mbali na hilo, lakini pia wakiwa vijana walishuhudia viongozi wa Serikali zote mbili wakiheshimu mpaka huo ndani ya ziwa , kwa kuwa hata waliposafiri toka upande mmoja kwenda mwingine kila wakifika eneo la Mto Songwe bendera ya upande mmoja ilishushwa na kupandishwa ya upande mwingine.
Philipo Mwandemele(73) kabla ya kuanza kutoa maelezo yake alitoa  kitabu kimoja kinachozungumzia maisha na desturi za wakazi wa nchi hizi mbili kama nyaraka muhimu  inayoweza kutumika kueleza ukweli juu ya sakata hilo la mpaka.

HII NDIO HALI ILIYOSABABISHWA NA KIMBUNGA SANDY MJINI NEW YORK

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

KUZIMA SIMU BANDIA UGANDA HADI MWAKANI

.
Uganda imeamua kusitisha mipango yake ya kuzima simu bandia hadi tarehe moja mwezi Julai mwaka 2013.
Hatua ya serikali inayolenga kuzuia simu bandia kutumika katika mitandao ya simu nchini humo ilikuwa imepangiwa kuafikiwa mwishoni mwa mwezi huu.
Lakini Kenya iliweza kuchukua hatua sawia na hii mwezi Oktoba na kuzima simu za zaidi ya watu milioni moja.

BAADHI YA PICHA ZA BONDIA WA TZ ALIYEPIGWA JANA.


TUME YA KATIBA IMEKUJA NA HII.

Photo: Jumapili Oktoba 25, 2012: Wananchi wa Bumbwini Misufini Shehia ya Bumbwini Misufini Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa kaskazini Unguja wakifuatilia kwa makini mkutano wa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Wilayani humo.Katika mchakato wa kukusanya maoni kuhusu katiba mpya, Tume ya kukusanya maoni imekuja na namba ambazo wananchi wanaweza kutuma maoni yao kwa njia ya sms, namba zenyewe hizi hapa
 0715 08 15 08, 0767 08 15 08, 078708 15 08, 077408 15 08.

HILI NDIO JESHI NCHINI NIGERIA LINALOKIUKA HAKI ZA BINADAMU.

Jeshi la Nigeria limetuhumiwa kufanya vitendo vya kukiuka haki za bindamu katika harakati zao dhidi ya kundi haramu la Boko Haram.
Madai haya yametolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.
Msemaji wa jeshi la Nigeria amekanusha madai hayo akisema kuwa wanajeshi hufanya kazi yao kwa kuzingatia sheria.
Harakati za kundi la Boko Haram, wanaopigania sheria za kiisilamu pia zimesababisha vifo vya mamia ya watu mwaka huu.
Wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara kaskazini mwa Nigeria na maeneo ya kati mwa Nigeria mwaka 2009.
Katika ripoti yake shirika la Amnesty limelaumu Boko Haram kwa visa vingi vya ukiukwaji wa haki za binadamu mauaji, kuteketeza makanisa na shule na mashambulizi yao dhidi ya waandishi wa habari.
Lakini ilisema kuwa hatua za jeshi dhidi ya kundi hilo zimechochea hali ya vurugu kuwa mbaya zaidi.

STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO TAR 1 NOV HIZI HAPA.

Kama hukupata matokeo ya kombe la Capital One Cup jana tar 31, haya hapa.



Chelsea5 - 4Manchester United

Norwich City2 - 1Tottenham Hotspur

Liverpool1 - 3Swansea City

RUSHWA YAIBUKA BUNGENI


MMOJA wa Wenyeviti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu pamoja na makada wengine wa CCM, juzi usiku walikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma kwa tuhuma za rushwa.

Zilizosomwa zaidi