Monday, October 29, 2012

KAMA HUKUONA PICHA ZA UFUNGUZI WA TREN DAR, HIZI HAPA


PANYA KAMA BINADAM





.Huyo ni panya anayepatikana mkoani Morogoro katika chuo kikuu cha Sokoine ambapo hutumika katika kutambua mtu aliyeathirika na TB. Panya huyo hutambua kwa kunusa makohozi ya mtu.
Kwa  sasa panya hao wanhudumia hospitali 13 nchini.

VIKAO VYA BUNGE DODOMA KUANZA LEO.

WAKATI Bunge likianza mkutano wake wa Tisa leo, zipo taarifa kuwa ripoti ya Kamati  ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wabunge kujihusisha na vitendo vya rushwa haitasomwa na kisha kujadiliwa.
Badala yake Kamati ya Uongozi, iliyokutana jana iliamua kwamba litatolewa tamko kuhusu ripoti ya kamati hiyo, hivyo haitasomwa wala kujadiliwa kama ambavyo wabunge wamekuwa wakitaka.
Kwa maana hiyo Spika wa Bunge, Anne Makinda huenda akatumia kanuni nyingine kutoa tamko kuhusu uchunguzi huo, hali ambayo haitatoa fursa kwa wabunge kuijadili kama ambavyo baadhi yao wamekuwa wakishinikiza.
Miongoni mwa kanuni ambazo Spika anaweza kuzitumia ni pamoja na ile ya 33 (2) ambayo inasema: “Wakati wa kikao, Spika anaweza kutoa taarifa nyinginezo kadri atakavyoona inafaa.”
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel jana alikataa kuzungumzia suala hilo akiahidi kulitoa ufafanuzi leo... “Ratiba ya shughuli za Bunge bado iko kwenye ngazi ya Kamati ya Uongozi. Sasa pengine tusubiri kesho (leo) ikiwa tayari kila kitu kitakuwa wazi, hakuna haja ya kuwa na haraka.”

MICHUANO KIKAPU IMEANZA LEO HUKO TANGA.

Michuano ya kikapu kombe la taifa imeanza leo huko
jijini Tanga  katika kiwanja cha CCM Mkwakwani
ambapo timu ya Tanga imekipiga na timu kutoka Pwani
na mchezo wa pili umekuwa kati ya Arusha na Lindi.
Katibu msaidizi wa shirikisho ls kikapu Tanzania TBF
Michael Malue amesema maandalizi yako vizuri sana
na mambo ni mazuri,
Amesema timu kutoka mikoa 13 zimeshawasili jijini Tanga.

Ratiba ya Michuano ya Capital One Cup kesho hii hapa.

Michezo yote ni saa 07:45 pm

          











Leeds UnitedvSouthampton

ReadingvArsenal

SunderlandvMiddlesbrough

Swindon TownvAston Villa

Wigan AthleticvBradford City








STORY ZA P SQUARE KUHUSU KIFO CHA MAMA YAO IKO HAPA.

Mapacha wa kundi la P-Square la nchini Nigeria hatimaye wamefunguka kuzikanusha tetesi kuwa walimtoa kafara mama yao mzazi ili watajirike na kufanikiwa zaidi kimuziki.


Katika mahojiano exclusive na gazeti la Vanguard la nchini Nigeria, Peter na Paul wamesema,


“Basi, ni mbaya sana kusikia kuwa watu wanatushutumu kwa kuhusika na kifo cha mama yetu. Hatumlamu mtu yeyote. Watu wako huru kusema chochote wanachotaka kusema. Tunashangaa kama kuna kitu chochote kitakachotufanya tuchukue maisha ya mama yetu mpendwa.

Maisha yake hayawezi kupimwa kwa fedha na umaarufu. Hivyo jibu letu kwa swali hili ni kwamba hatuhusiki na kifo cha mama yetu. Tunakilaumu tu kifo kilichomchukua mbali nasi ambacho kama si chenyewe watu wasingekuwa wanatunyooshea vidole. Alifariki baada ya ugonjwa wa muda mfupi.”

TRENI IMEANZA SAFARI NDANI YA DAR.

HATIMAYE usafiri wa treni ndani yaT Jiji la Dar es Salaam kuanza rasmi leo na kupokewa kwa furaha na wananchi waliojitokeza kuutumia. Waziri mwakyembe ameonekana ndani ya gogo akifurahia kuzinduliwa kwa usafiri huo

Matokeo Barclays Premier League jana tar 28 yalikuwa hivi


Everton2 - 2Liverpool

Newcastle United2 - 1West Bromwich Albion

Southampton1 - 2Tottenham Hotspur

Chelsea2 - 3Manchester United

STORI KWENYA MAGAZETI YA LEO TAR 29 OCT HIZI HAPA

WAZIRI MEMBE AENDELEA NA UCHUNGUZI

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe yuko mkoani Mbeya kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni mwendelezo wa kutembelea mikoa na vitongoji vilivyopo katika fukwe za Ziwa Nyasa.

Zilizosomwa zaidi