Tuesday, October 23, 2012

Barack Obama na Mit Romney kwenye mdaharo wa mwisho.

 MDAHALO WA MWISHO WA WAGOMBEA WA URAIS

Nani msema ukweli? Nani amewashawishi wapiga kura vya kutosha kabla ya uchaguzi? Ni Obama au Romney?

Wagombea katika uchaguzi mkuu wa Marekani Barack Obama na Mit Romney wametofautiana kuhusu sera ya kigeni,Obama akisema Romney hana uelewa wowote wa sera ya kigeni wakati Romney akisema Obama alikosea katika sera yake ya Mashariki ya kati. Kwamba amesababisha vurugu zaidi tangu aingine madarakani.

YANGA KUKIPIGA NA POLISI MOROGORO KESHO UWANJA WA TAIFA.


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Kocha mkuu wa timu ya Young Africans Sports Club, Mholanzi Ernie Brandts amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili timu ya Polisi Morogoro katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom utakaofanyika kesho uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akiongea katika mtandao wa klabuhiyo leo asubuhi katika mazoezi yaliyofanyika shule ya sekondari Loyola, amesema wachezaji wake wote wapo safi, wana ari ya mchezo na ushindi, hivyo anaamini mchezaji yoyote atakayempanga atafanya vizuri.

Polisi Morogoro timu iliyoipanda ligi msimu huu 2012/2013 inakamata mkia katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom ikiwa na pointi 2 ilizozipata kwa kutoka sare michezo miwili kati ya michezo saba iliyokwishacheza.
 
Yanga ambayo mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki, itaingia uwanjani kusaka pointi 3 muhimu zitakazo isogeza mpaka nafasi tatu za juu na kupunguza tofauti ya point na mtani wake wa jadi Simba anayeongoza ligi kwa pointi 19.
 
Katika mazoezi yaliyofanyika leo asubuhi, kocha Brandts ameendelea kufurahia kuwepo kwa wachezaji wake wote, kitu kitakachopelea kumtumia mchezaji yoyote atakayetaka kumtumia kwa mchezo huo wa kesho, kwani hakuna mchezaji aliye majeruhi .
 
Vijana wa jangwani kwa sasa wanakamata nafasi ya tatu katika msimao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa kufikisha point 14 nyuma ya Azam yenye pointi 17 na Simba yenye pointi 19 ikiwa mbele kwa mchezo mmoja. 

Mchezo utaanza majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na viingilio vya mchezo huo ni:
 
VIP A 20,000/=
VIP B &C 15,000/=
Orange 8,000/=
Blue & Green 5,000/=

STORI YA LORD EYES IKO HAPA.



Lord Eyes
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela amethibitisha jeshi lake kumshikilia msanii Lord Eyes ambae toka weekend iliyopita taarifa zake zimesambaa baada ya kushutumiwa kuhusika na wizi wa vifaa mbalimbali kwenye gari la mwimbaji Ommy Dimpoz.

Kamanda huyo alisema “ni kweli Isaac Waziri Maputo mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa tarehe 20 mwezi wa kumi usiku maeneo ya Kinondoni, kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu ni kutokana na taarifa tulizozipata kupitia kwa binti mmoja aitwae Kurushinde Hillary (22) mwenye asili ya kiburushi lakini mkazi wa Mwananyamala kwa Makoma Dar es salaam, alikamatwa siku hiyo hiyo kabla ya Lord Eyes”

“Alikamatwa kuhusiana na matukio ya wizi kwenye magari yani kuna mtindo ambao umeibuka ambapo ukipaki gari yako gari nyingine ya wezi inakuja inapaki jirani na gari yako ambapo kwa muda mfupi wanafanya utundu wao wanaoujua, wanafungua gari na kuiba mali iliyoko ndani, mara baada ya huyu binti kukamatwa katika kuhojiwa mtandao wake anaoshirikiana nao alimtaja mtuhumiwa Isaac Waziri Maputo (Lord Eyes)”


Kwenye sentensi nyingine Kamanda Kenyela amesema “watu wengi wamelalamika kuibiwa laptop zao, mabegi, mifuko na hata silaha kwa maana mtu anakua anajiamini anaacha kwenye gari akiamini kwamba ameshalock lakini watu hawa na mtandao wao wamekua ni hatari kiasi kwamba wameliza watu wengi”

“Watuhumiwa hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo 30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza yakaongezeka ambayo yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama vile Mlimani City, Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach,


  kwenye kumbi mbalimbali za starehe na pia  kwenye maeneo ambayo kunakua na harusi, sehemu ambazo kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya wizi”

KAMA ULIMISI STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO HIZI HAPA.

Zilizosomwa zaidi