Thursday, October 18, 2012

ALIYOONGEA KOCHA WA SIMBA KUHUSU KIBADENI.

Milovan amkubali King Kibadeni 

,BAADA ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Kagera Sugar juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kocha mkuu wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovik, amekisifu kiwango cha wakata miwa hao.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Milovan alisema kuwa Kagera kipindi cha pili ilionyesha kandanda safi na la kuvutia hadi kuwafunika wachezaji wake, ambao walionekana kuzidiwa kasi.
“Kagera wamecheza soka safi na hasa katika kipindi cha pili na kuwazidi wachezaji wangu, ambao kutokana na makosa kadhaa waliyoyafanya, walitoka sare ya mabao 2-2,” alisema Milovan huku akimpa mkono wa hongera, kocha mkuu wa Kagera Sugar, Abdallah ‘King’ Kibadeni.

KANISA LA KKT LATOA TAMKO.

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, limedai kushangazwa kwake na ukimya wa serikali pamoja na vyombo vya dola kwa kutochukua hatua mapema za vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyokuwa vikitendeka.
Kanisa hilo pia limeeleza kusikitishwa kwake kwa vitendo vya uchomaji wa makanisa wakieleza kuwa kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha kifo cha Baba wa Taifa ni kebehi kwa watu waliokalia kiti chake.
Akizungumza katika ibada maalumu na kutoa salaamu za maaskofu wa kanisa hilo nchini kote kuhusiana na matukio ya kuchoma moto makanisa ya Kikristo, iliyofanyika katika kanisa la jimbo kuu Kusini Mbagala, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, alisema kuwa wamekutana kwa madhumuni ya kuonyesha majonzi yao kwa vitendo vya uvunjifu wa amani walivyoviita ni kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa Watanzania.
Shao pia alisema kuwa madhumuni mengine ni kupokea matumaini ya Tanzania mpya katika msiba wa wenye dini na wasio na dini.

HABARI KUHUSU KUUAWA KWA ASKARI ZANZIBAR HII HAPA.

Habari ifuatayo imeandikwa na Ramadhan Ali na Mwanaisha Mohammed
Askari mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi wakati akirudi kazini majira ya saa 6.30 usiku katika eneo la Bububu. 

 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema mauaji hayo yamesababishwa na fujo za wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO baada ya kuenea uvumi wa kutekwa Msemaji Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid Hadi usiku wa kuamkia jana.

 Kamishna Mussa amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu waliofanya mauaji ya Coplo Saidi Abdulrahaman ili kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani kama sheria za nchi zinavyowaelekeza. 

 Amesema mpaka hivi sasa watu 10 wamekamatwa kwa tuhuma za makosa mbali mbali yaliyotokana na vurugu za jana na upelelezi wa kujua ukweli juu ya uvumi wa kutekwa Sheikh Farid unaendelea.

 Ameongeza kuwa kutekwa kwa Sheikh Farid kunatia mashaka kutokana na mazingira ya kutoweka kwake kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mdogo wake Said Omar Said ambae alikuwa dereva wake katika hatua za mwisho maeneo ya Mazizini walipokwenda kununua umeme.

 “Sheikh Farid alimuamuru Said amuache katika eneo hilo aende nyumbani kupeleka umeme na wakati huo akaendelea na mazungumzo na watu wengine walikuwemo ndani ya gari nyengine ndogo ya NOAH ambayo nambari zake hazijajulikana lakini aliporudi kumchukua hakumkuta” alisema Kamishana Mussa.

 Amesema fujo hizo zilisababisha hasara kubwa kwa Serikali, Chama tawala na wananchi ikiwemo kuchoma na kuharibumiundo mbinu ya barabara, kuharibu maskani za CCM za Kisonge na Muembeladu kwa kuzichoma moto baadhi ya magari kuvunjwa vioo na kuvunja duka la pombe na kuiba mali iliyokuwemo ndani.

 Hata hivyo amedai hali ya Mji wa Zanzibar kwa sasa ni shwari, wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikosi vyengine vya ulinzi na usalama vitaendelea kuhakikisha amani inadumu muda wote. 

 Amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu na kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao, na kutoa taarifa za watu waliohusika na vurugu pamoja na mauaji ya Coplo Said Abdulrahaman.

PICHA MBALIMBALI ZA PONDA AKIWA MAHAKAMANI.

Picture Picture Picture Picture Picture Picture Picture Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu(T), Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake 49 jana wakishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam chini ya ulinzi mkali wa wanausalama kwa kosa la uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Shilingi milioni 59.

AFARIKI BAADA YA HARUSI.



 Bi. Agnes Wathanu akimvisha pete mumewe Bw.Peter Muchoki wakati wa ndoa

RWANDA KUWA MJUMBE UNO

Rwanda imechaguliwa kuwa mjumbe wabaraza la usalama wa mataifa.


RWANDA NA KUCHAGULIWA UNO

                                                    Rwanda imechaguliwa kuwa mjumbe katika umoja wa mataifa

Moto umelipuka katika hifadhi mkoani Singida

STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO HIZI HAPA.

Polisi waendelea kuiimalisha ulinzi huko kisiwani Zanzibar.
ITV imeripoti hayo katika habari za saa mchana wa leo.

Zilizosomwa zaidi