Wednesday, October 17, 2012
MGAMBO MBIO KALI, SIMBA, AZAM KIMYA.
MGAMBO Shooting wameendeleza wimbi lake la ushindi kwa kuichapa Toto
African kwa mabao 2-0, huku Simba ikitoka sare na Kagera Sugar huku Azam nayo ikitoka sare na Tanzania Prisons.
Kwa ushindi huo umeifanya
Mgambo Shooting kupanda hadi nafasi ya 8 ikiwa na pointi 9 katika
msimamo huo unaoongozwa na Simba wenye pointi 18 wakifuatiwa na Azam
(17) na JKT Oljoro (13).
Mgambo Shooting iliyopanda daraja msimu
huu imeweka rekodi ya kushinda mechi yake ya tatu mfululizo baada ya
kuanza ligi kwa kusuasua ikiwa imepoteza michezo mitano kabla ya
kushinda dhidi ya Polisi Moro na Mtibwa Sugar.
Mgambo Shooting wakiwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani walipata bao la kuongoza katika dakika ya 58 kupitia kwa Full Maganga aliyeunganisha kwa kichwa pasi iliyopigwa na Yasin Awadhi kabla ya Issa Kanduru kupachika bao la pili katika dakika ya 62 akiunganisha kona iliyopigwa na Salum Kipanga na kuichapa Toto African 2-0.
Nao mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wameendelea kusuasua baada ya kupoteza pointi nne katika michezo miwili mfululizo kufutia sare yao dhidi ya Coastal Union na Kagera Sugar.
Mgambo Shooting wakiwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani walipata bao la kuongoza katika dakika ya 58 kupitia kwa Full Maganga aliyeunganisha kwa kichwa pasi iliyopigwa na Yasin Awadhi kabla ya Issa Kanduru kupachika bao la pili katika dakika ya 62 akiunganisha kona iliyopigwa na Salum Kipanga na kuichapa Toto African 2-0.
Nao mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wameendelea kusuasua baada ya kupoteza pointi nne katika michezo miwili mfululizo kufutia sare yao dhidi ya Coastal Union na Kagera Sugar.
VURUGU YA AJABU DAR NA ZANZIBAR
POLISI mkoani Dar es Salaam na wale wa Kisiwani Zanzibar, jana walitumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kusambaratisha makundi ya watu wanaodaiwa kuwa waumini wa Dini ya Kiislamu, waliopanga maandamano kushinikiza kuachiwa kwa viongozi wao.
Kisiwani Zanzibar vurugu kubwa ziliibuka baada ya kusambaa taarifa kuwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed alitekwa nyara juzi saa 3 usiku akiwa kwenye gari lake na dereva wake.
Vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa mali kadhaa ikiwamo Maskani Kaka ya Kisonge inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo ilichomwa moto na waandamanaji.
Waandamanaji hao pia walichoma moto baa za Darajani na Mbawala eneo la Mikunguni na baadhi ya nyumba za kulala wageni, kabla Vikosi vya Kutuliza Ghasia (FFU) na Kikosi cha Zima Moto kudhibiti vurugu hizo kwa mabomu ya kutoa machozi.
Pia magari kadhaa yalichomwa moto na kuharibiwa vibaya yakiwa yameegeshwa katika maeneo mbalimbali, huku mipira na matairi vikichomwa katika barabara kadhaa.
Katika maeneo ya Mjini baadhi ya njia zilifungwa na watu waliokuwa wakitoka kazini walishindwa kwenda nyumbani. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale ya Malindi, Darajani hadi Michenzani ambako njia zilifungwa na mabomu yalisikika yakipigwa mfululizo.
Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheik Abdallah Said alisema,
“Taarifa tulizonazo ni kwamba Sheikh Farid ametoweka katika mazingira ya kutatanisha…Alitoka kwake Mbuyuni katika gari yeye na kijana wake wa hapo nyumbani, lakini baadaye kuna gari ikamfuata na kusimama na ndipo alipoingia katika hilo gari jingine na hakuonekana tena. Hatujui ni kina nani waliomchukua na hatujui ilikuwaje akaingia katika hilo gari ...”
Polisi waliimarisha ulinzi katika baadhi ya maeneo hasa Msikiti wa Mbuyuni ambao uko jirani na makazi ya Sheikh Farid. Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema polisi halihusiki na kukamatwa kwa Farid, lakini wao wanaamini kwamba ‘amejipoteza’ mwenyewe na kujificha.
MWENYEKITI MBEYA ANUSURIKA KUUAWA.
MWENYEKITI wa Chama cha Albino Tanzania (TAS) Mkoa wa Mbeya,
Sinzo Dereva (38) ambaye ni mlemavu wa ngozi amenusurika
kuuawa baada ya watu watano wasiofahamika kuvamia nyumbani kwake kwa nia ya kumfanyia uhalifu.
TANZANIA NA MALAWI TENA.
Baada ya mvutano wa hapa na pale, Serikali
ya Malawi imekubali kurudi katika
meza ya mazungumzo kuhusu mgogoro wa
mpaka katika Ziwa Nyasa kati yake
na Tanzania. Hii yoteni katika kutafuta suruhu kwa njia ya amani
ALIYOSEMA DK ULIMBOKA.
Katika waraka uliowasilishwa hapo jana, Dk Ulimboka anaihoji Serikari ni
hatua gani imechukua katika kufanya uchunguzi tangu alipote alipotekwa na
kupigwa vibaya sana. Katika waraka huo uliosomwa na mwanasheria a
liyemchagua yeye mwenyewe amemtaja mfanyakazi mmoja wa ikulu
ambaye aliiwasiliana naye kwa mara ya mwisho siku hiyo ya tukio.
Kama haukumbuki, hizi ni baadhi ya Picha baada ya kutekwa
na kupigwa vibaya kwa Daktari huyo.

kupigwa vibaya sana. Katika waraka huo uliosomwa na mwanasheria a
liyemchagua yeye mwenyewe amemtaja mfanyakazi mmoja wa ikulu
ambaye aliiwasiliana naye kwa mara ya mwisho siku hiyo ya tukio.
na kupigwa vibaya kwa Daktari huyo.
OBAMA na ROMNEY KWENYA MDAHALO.
Hapa ni mdahalo uliofanyika jana nchini mMarekani kati ya
Barack Obama na mshindani wake Mitt Romney wa Republican
Afrika Kusini na ubaguzi wa rangi.
Vijana wa kike na wa kiume nchini Afrika kusini wakifurahia kwa pamoja
katika siku ya kuadhimisha kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.
katika siku ya kuadhimisha kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Israel Magesa Wakili Magesa aliyeko (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi. Wakili Magesa, ambaye ni mmiliki wa kampuni y...
-
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu. ...
-
-
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bo...
-
Nimepokea mwaliko wa kikao maalumu cha kikao cha fedha na uongozi wa tarehe 3/01/2014 kikao kufanyika tarehe 06/01/2013 saa nane mchana ...
















