Monday, October 15, 2012
WEMA SEPETU, AUNT EZEKIEL KUJISAFISHA.
WAAMUA KUOMBA RADHI KUTOKANA NA PICHA CHAFU WALIZOPIGA WAKATI WA FIESTA
Waigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamewaomba radhi watanzania kwa picha zao mbaya walizopigwa kwenye show za Fiesta.
Wasanii hao wamezungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuomba radhi kwa kupigwa picha hizo za nusu utupu walizopigwa kwenye show hizo.
Aunty Ezekiel amesema ameumizwa na kitendo hicho kwakuwa wao kama wanawake katika jamii, wana wazazi, ndugu jamaa, marafiki pamoja na mashabiki wao wanaowapenda na kuwaheshimu.
Hivi karibu Aunty Ezekiel alijitetea na kunukuliwa kwenye chanzo kimoja akisema, “Ni kweli nilikuwa ninacheza katika Jukwaa (Stage) na nilikuwa nimekunywa, lakini sikuwa nimedhamiria kukaa uchi bali ni mbinu za wapiga picha ambao walitumia njia ya kuamua kunidhalilisha kwa kunipiga picha wakiwa chini ya Jukwaa (Stage) ili wapate kuuza magazeti yao, hata ukiangalia picha zenyewe zimepigwa kiujanja sana.”
MAUAJI YA KULIPIZA KISASI KENYA.

(Wanachama wa MRC)
Afisaa mmoja
nchini Kenya ameuawa katika kile polisi wanachodai kuwa ni shambulizi la
kulipiza kisasi kufuatia kukamatwa kwa kiongozi wa vuguvugu la MRC
(Mombasa Republican Council) mjini Mombasa, nchini Kenya.
kwa mujibu
wa polisi, Salim Changu ambaye ni naibu chifu wa eneo hilo
alinyongwa nyumbani kwake katika eneo la Kwale mjini Mombasa,
Kifo chake kilitokea baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa vuguvugu hilo linalotaka kujitenga na eneo la Pwani ya Kenya.
PICHA ZA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA RPC MWANZA, LIBELATUS BARLOW.
HIZI NDIO PICHA ZA LEO KATIKA UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA
KWENYE SHUGULI NZIMA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU BARLOW.
(Picha zote Elia Migongo)

Maafisa wa polisi , wakiuingiza uwanjani mwili wa Kamanda Barlow

Maafisa wa polisi wakiuweka sawa mwili wa Kamanda Barlow

Marehemu ASCP Barlow akiwa amelazwa katika jeneza

Fr Anthony Manyanga , akiongoza Misa takatifu ya kuaga mwili wa marehemu
Waziri wa
nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge Wilium Lukuvi (katika)
kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa mwanza Eng. Evarist Ndikilo, Kushoto ni
DCI Robert Manumba
| Waziri Lukuvi akiaga Mwili wa marehemu |
![]() |
| Naibu waziri wa uchukuzi Eng. Charles Tzeba, akitoa heshima za mwisho |
![]() | ||||||||||||||||||||||||||
| Mjane wa marehemu Kamanda Barlow , hapa akitoa heshima za Mwisho mbele ya mwili wa marehemu |
Subscribe to:
Posts (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Israel Magesa Wakili Magesa aliyeko (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi. Wakili Magesa, ambaye ni mmiliki wa kampuni y...
-
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu. ...
-
-
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bo...
-
Nimepokea mwaliko wa kikao maalumu cha kikao cha fedha na uongozi wa tarehe 3/01/2014 kikao kufanyika tarehe 06/01/2013 saa nane mchana ...

















