Sunday, October 14, 2012

Rais wa Mauritania apigwa risasi.


Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, amepelekwa Ufaransa kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa alipopigwa risasi.


Kabla ya kuondoka kuelekea Paris, Rais Abdel Aziz alisema kwenye hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni kutoka hospitali, kwamba ameshafanyiwa upasuaji ambao ulifanikiwa.
Wakuu walisema rais alijeruhiwa wakati wanajeshi wa serikali waliokuwa kwenye doria, walipofyatulia risasi msafara wa rais.
Rais wa MauritaniaInaarifiwa kuwa maafisa wawili wa jeshi wamekamatwa.
Jenerali Abdel Aziz, ambaye anaonekana na mataifa ya magharibi kuwa anasimama dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika eneo hilo, alichaguliwa mwaka wa 2009, mwaka mmoja baada ya kupindua serikali.

WAUAWA WAKITOKA MSIKITINI.


Watu wauwawa Nigeria wakitoka msikitini

Kijiji cha Dogo Dawa kwenye ramani Nigeria imeripoti  kuwa watu waliokuwa na silaha wamewauwa takribani watu 20 katika shambulio lilofanywa alfajiri kwenye kijiji cha Dogo Dawa katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa nchi.
Waliouwawa walikuwa wakitoka msikitini.
Washambuliaji walifyatua risasi na kuwapiga visa.
Afisa habari wa jimbo hilo, Saidu Adamu, ameripoti  kwamba gengi la majambazi wa jimbo hilo walifanya mauaji hayo.

KAMA UMEMISI STORI ZA MAGAZETI YA LEO, HAYA YANAKUHUSU.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI NA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA NA MAENEO JIRANI

Jeshi la police mkoa wa mwanza linawaalika ndugu jamaa na marafiki kuuaga mwili wa marehemu kamanda wa polisi mkoani Mwanza bwana Liberatus Barlow,zoezi hilo litafanyika kesho tarehe 15/10/2012 jmatatu asubuhi kuanzia saa 08:00am (saa mbili asubuhi) hadi saa 01:00pm (saa saba mchana) katika viwanja vya nyamagana jijin mwanza.

Zilizosomwa zaidi