Saturday, October 13, 2012

SKENDO ZA WATOTO WA VYUO VIKUU NCHINI.


Mmomonyoko wa maadili katika vyuo vikuu  hapa nchini umekuwa ukisababishwa na ugumu wa maisha  na kucheleweshwa  kwa hela ya kujikimu toka bodi ya mikopo ya elimu ya juu hapa nchni na uongozi mbovu wa vyuo........

Wakiongea kwa nyakati tofauti na mtandao huu, baadhi ya wanafunzi hao toka vyuo mbalimbali wamedai kuwa maisha ya chuo ni magumu sana hasa kwa mtoto wa kike ambaye anahitaji vitu vingi ili aweze kujikimu kimaisha.......
"Kwa kweli maisha ya chuo ni magumu sana hasa kwetu sisi wasichana.Hela yetu ya kujikimu huchelewa sana.Wazazi nyumbani wanajua kuwa  tuna mkopo na wengine wanaimani finyu kuwa tunalipwa na serikali.......

Ukiomba hela nyumbani unagombezwa na hupewi au  wakikuonea huruma watakurushia  30,000  .Sasa hiyo hela inatosha kula, kununua mafuta,kusuka na vitu vingine?".......

Katika hali kama hii, inakuwa ni vigumu sana kwa mtoto wa kike kuvishinda vishawishi......Na ndipo  tunapolazima kutafuta sehemu ya kujihifadhi kwa wakaka......" Alieleza binti mmoja ambaye hivi sasa ni mwaka wa pili ( chuo tunakihifadhi)
Mbali na maoni hayo, mwanafunzi mwingine toka ukanda wa pwani alikuwa na mtazamo tofauti:

"Tatizo ni malezi ya kila mtu. Chuo na mapenzi havina uhusiano wowote.Mbona hata hata huko mtaani mapenzi yapo? Kwa nini wasilaumiwe wao?  Suala la msingi ni kwamba siku hizi uzushi mwingi.
Wanaume  wanatembea na simu zenye kamera. Ukilala  anakupiga picha alafu mkiachana anakuweka facebook."

Maoni ya huyu binti yalimfanya mwandishi wetu atake kujua zaidi  juu ya asili ya picha hizo za utupu maana zimekuwa zikipigwa katika pozi na si  kwa kuviziwa....

"Ni kweli baadhi yetu hufanya hivyo.Sasa hayo nimakubaliano yao.Pengine kaambiwa kwa kufanya hivyo atapewa hela ndefu zaidi na ukizingatia mfukoni hana kitu na  boom halitabiliki.Unadhani atafanyaje? .....
Kwa asilimia kubwa wasichana tupo katika wakati mgumu sana.Hata sisi hatupendi kupigwa tukiwa uchi ila  tunalazimika kutokana na mazingira"

MAKANISA YALIYOCHOMWA DAR YAFIKA SABA.


Wakati idadi ya makanisa yaliyochomwa moto  kutokana na vurugu zilizotokea juzi Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam ikifikia saba, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo wameonya kuwa, Serikali ikishindwa kudhibiti matukio ya vurugu za kidini, taifa linaweza kuingia katika umwagaji damu.Vurugu hizo zilitokea juzi baada ya watu wanaodaiwa kuwa waumini wa dini ya Kiislamu kuvamia Kituo cha Polisi, wakitaka wapewe  mtoto aliyedaiwa kudhalilisha kitabu kitakatifu cha Quran kwa kukikojolea.

KATIKA KUMBUKUMBU YA MIAKA 13 BAADA YA KIFO CHA MWL. NYERERE.


Julius Nyerere
Sote tunaweza kuwa maarufu, tunaweza kuwa chochote tunachotaka . Pamoja na hayo, jambo moja ambalo ni dhahiri itakuwa ni vigumu sana kulifikia ni kuwa maarufu na kuheshimika duniani kote kama ilivyokuwa kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye hivi leo tunakumbuka miaka kumi na moja (11) tangu afariki dunia mnamo tarehe kama ya leo mwaka 1999 kule nchini Uingereza katika hospitali ya Mtakatifu Thomas kwa ugonjwa wa saratani ya damu (leukemia).
Serikali ilipotangaza rasmi kwamba Nyerere hatunaye tena, uchungu na simanzi uliikumba nchi nzima na dunia kwa ujumla hususani kwa wale waliokuwa wanamjua Nyerere na kujua alichokuwa akikisimamia na alichokiamini. Bara la Afrika likawa limempoteza kipenzi chake, mtoto wa Afrika ambaye thamani ya mchango wake katika ukombozi wa bara la Afrika haina kipimo. Mpaka anafariki dunia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha amani barani Afrika.Mfano mzuri ni mgogoro wa Burundi aliokuwa akijaribu kuusuluhisha. Mwenyewe aliwahi kutamka kwamba yeye ni mwafrika kwanza na kisha mjamaa.
Mpaka leo hii jina la Nyerere linabakia kuwa kitambulisho chetu kikubwa .Wakati mwingine zaidi hata ya jina la nchi yetu yaani Tanzania.Wapo watu wanaolijua jina la Nyerere na wala wasijue jina la Tanzania au hata Tanganyika. Haishangazi, alikuwa ni mwana wa Afrika kamili. Kadiri siku zinavyopita, taratibu baadhi yetu, hususani vijana wanaoitwa wa kizazi kipya, wanazidi kulisahau jina la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Viongozi wetu wengi wa sasa( ingawa wakati wa msiba wake waliahidi kumuenzi kwa hali na mali) wanaelekea kusahau kabisa ahadi zao! Wengi wanabakia kumuenzi kwa maneno na sio vitendo.
Lakini je,sote tunafahamu japo kidogo tu historia ya Mwalimu Nyerere? Uwezekano ni kwamba sio wote,hususani vijana wa sasa. Kwa kifupi na kwa msaada wa vyanzo mbalimbali hii hapa historia fupi ya Hayati Baba wa Taifa;
Julius Kambarage Nyerere
Hayati Baba wa Taifa akisisitiza jambo
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13 Aprili mwaka 1922 huko Butiama mkoani Mara, pembezoni mwa ziwa Victoria,kaskazini mwa Tanzania. Baba yake alikuwa ni Chifu katika kabila dogo la Wazanaki.Nyerere alikuwa miongoni wa watoto wanaosemekana kufikia hadi 26. Baba yake, Mzee Burito Nyerere alikuwa na wake wapatao 22.Alianza shule akiwa na umri wa miaka 12 (ilimbidi kutembea kwa zaidi ya kilometa 26 hadi Musoma mjini ili kupata elimu ya msingi). Kipaji cha uelewa shuleni kilimuwezesha kumaliza kozi ya miaka minne ndani ya miaka mitatu tu. Baadaye mnamo mwaka 1937,alijiunga na shule ya sekondari ya serikali ya Tabora kwa masomo ya sekondari. Alibatizwa katika kanisa katoliki akiwa na umri wa miaka 20.
Kipaji chake cha kitaaluma na kiuongozi kilionekana tangu mapema. Kwa msaada wa waliokuwa waalimu wake pale Tabora (ma-father wa kanisa katoliki) baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda kusomea ualimu. Fikra za kimapinduzi na kusaidia waafrika wenzake zilianza kuonekana wazi akiwa Makerere.
Nyumba ya Nyerere
Nyumba aliyojengewa Mwalimu Nyerere na serikali baada ya kustaafu.Ipo Butiama.
Baada ya kumaliza Makerere alirejea Tanzania na kwenda kufundisha (St. Mary’s Secondary School) mkoani Tabora. Mwaka 1949 alipata scholarship kwenda Chuo Kikuu cha Edinburgh kusomea shahada ya pili (Masters) katika historia na uchumi wa kisiasa(History and Political Economy). Alipokuwa masomoni Edinburgh, Nyerere ndipo alipoanza rasmi kuunda mawazo yake ya kiukombozi kufuatia kuanza kujifunza kilichoitwa Fabian Thinking . Mawazo yake ya kuunganisha ujamaa na ujima au maisha ya kijamii ya kiafrika ndipo yalipoanza kujijenga au kujiimarisha.Harakati za kujipatia uhuru kwa nchi ya Ghana zilizokuwa zikiongozwa na Dr.Kwame Nkrumah,anakiri Nyerere katika baadhi ya mahojiano aliyowahi kufanya, zilichangia kuamsha fikra za kujikomboa kutoka mikononi mwa wakoloni. Inasemekana Nyerere ndio alikuwa mtanzania wa kwanza kusomea katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata degree nje ya Afrika. Alihitimu mwaka 1952.
Nyerere na mama Maria
Mwalimu Nyerere na mkewe Mama Maria Nyerere.
Aliporejea nchini Tanzania (enzi hizo bado ikiitwa Tanganyika), alianza kazi ya kufundisha masomo ya Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St.Francis’ (sasa Pugu Sekondari). Wakati huo huo akawa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa TAA(Tanganyika African Association) chama kilichokuwa kimeundwa kusimamia maslahi ya waafrika ingawa tayari kikiwa na vuguvugu la kiukombozi na kisiasa. Hapo ndipo serikali ya kikoloni ilipomlazimisha kuchagua kati ya kufundisha(ualimu) au siasa. Mwenyewe anasema alikuwa amepanga kufundisha kwa angalau miaka mitatu kwanza kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye siasa. Hilo halikuwezekana. Akachagua kuwa mwanasiasa na hivyo kuanza mkakati mzito wa kuviunganisha vyama mbalimbali vilivyokuwa na malengo sawa.
Nyerere was a simple man!
Mwalimu Nyerere ndani ya Butiama.
Kazi ya kuviunganisha vikundi mbalimbali vya kisiasa vilivyokuwa vimeanza kutapakaa nchi nzima haikuwa rahisi. Lakini alifanikiwa kufanya hivyo mwaka 1954 kwa kuundwa kwa TANU(Tanganyika African National Union) na yeye kuchaguliwa kukiongoza.
Humo ndimo alimopumzika Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.Tizama na tafakari kwa makini maneno yaliyoandikwa hapo nje.
Aliingia katika bunge la wakati huo mwaka 1958 kabla hajawa waziri mkuu mwaka 1960. Tarehe 1 May 1961, Tanganyika ilipewa uhuru wa kujitawala na Nyerere akawa waziri mkuu wa kwanza. Uhuru kamili ulipatikana mwaka tarehe 9 December 1961. Mwaka mmoja baadaye (1962) Nyerere akawa Raisi wa kwanza wa Tanganyika ilipokuwa Jamhuri ya Tanganyika.
Nyerere,mama yake na mkewe
Mwalimu Nyerere(katikati),mama yake mzazi(kushoto) na mkewe Maria(kulia).Picha hii ilipigwa Novemba 10,1985 Butiama baada ya Nyerere kustaafu.
Julius Nyerere alimuoa Maria Gabriel Magige (Mama Maria Nyerere) tarehe 24 Januari 1953 na walijaliwa kupata watoto wanane. Alipostaafu nafasi yake ya uraisi mwaka 1985 alirudi kijijini Butiama ambako alibakia kuwa mkulima wa kawaida mpaka kufariki kwake Oktoba 14, 1999. Endelea kupumzika kwa amani Mwalimu.
Tanzania note
Sura ya Nyerere katika noti ya Shs 100 enzi hizo.
R.I.P MWALIMU JULIUS K.NYERERE.


MABONDIA WAPIMA UZITO LEO JIJINI DAR




Bondia THOMAS MASHALI kushoto akitunishiana misuri na MEDY SEBYALA wa UGANDA baada ya kupima uzito Dar es salaam leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa katika pambano la Ubingwa wa Africa mashariki litakalofanyi ukumbi wa Friends corner hotel siku ya jumapili 14/10/2012a katika anaeshudia katikati ni Rais wa TPBC Onesmo Ngowi ambaye ndie msimamizi mkuu wa mpambano huo

Matokeo ligi kuu Tanzania Simba Sc V/S Coastal Union

Dakika 90 za mchezo
Simba Sc 0-0 Coastal Union

VURUGU ZA JANA DAR.

ENEO la Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam jana liligeuka uwanja wa mapambano kati ya makundi ya article thumbnailwatu wanaosadikiwa kuwa ni Waislamu na polisi baada ya watu hao kuvamia Kituo cha Polisi Kidogo cha Maturubai kilichopo eneo hilo.
Watu hao walivamia kituo hicho wakitaka wakabidhiwe mtoto anayedaiwa kukojolea kitabu kitakatifu cha Quran ili wamwadhibu.
Vurugu hizo zilizoanza tangu saa nne asubuhi, zilisababisha makanisa matano kuchomwa moto, magari kadhaa kuvunjwa vioo na watu hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime alisema watu kadhaa wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo... “Siwezi kutaja idadi ya waliokamatwa, lakini kuna watu tunawashikilia kutokana na kufanya fujo, kwa sasa niko katika operesheni, nitazungumza kwa kirefu baadaye.”

Hii ndio hali halisi ya watoto wa mtaani jijini Dar.

SERIKARI YA TANZANIA YAFIKISHWA MAHAKAMA YA THE HAGUE

.
Hatua hiyo ya LHRC inatokana na ripoti tatu zilizotolewa  hivi karibuni kuchunguza kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi kilichotokea katika Kijiji cha Nyololo, Mkoa wa Iringa, Septemba 2 mwaka huu.
Ripoti hizo ni ile ya Kamati ya Kuchunguza Mauaji hayo iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi iliyokuwa chini ya Jaji Steven Ihema; Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyokuwa chini ya Jaji Kiongozi Mstaafu, Amir Manento na ile ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef), iliyoongozwa na John Mirenyi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Helen Kijo-Bisimba alisema kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, jumla ya watu 24 wameuawa na watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama.
“Tumepeleka mashtaka 24 ICC tangu Septemba 28 mwaka huu, ambayo yanahitajika kufanyiwa uchunguzi na kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikiwalinda viongozi wake wanaokiuka haki za binadamu,” alisema Dk Bisimba.
Alisema taarifa hizo pia wamezipeleka kwenye Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu katika kikao kinachoendelea huko Ivory Coast, lengo likiwa ni kuchunguza na kuchukua hatua katika Mahakama ya Afrika.
“Tunatarajia kuona uwajibikaji wa viongozi wote wa Serikali na vyombo vya dola waliohusika kwa njia yoyote ile. Hatua hizo au uwajibikaji huo ni pamoja na kujiuzulu, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani, ” alisema.
Aliitaka Serikali kuacha propaganda zinazotaka kuchochea vurugu katika taifa huku akisema inapaswa itambue kuwa hivi sasa nchi iko katika zama za vyama vingi vya siasa na kuacha kutumia vyombo vya dola kuleta chuki na mafarakano.
Dk Bisimba alisema baada ya kupitia taarifa zote tatu, LHRC kimesikitishwa na taarifa ya Kamati ya Dk Nchimbi... “LHRC hakijashangazwa sana pale taarifa hiyo ilipoonyesha wazi nia ya kuwalinda watuhumiwa kwa kuwa Serikali yetu bado haijajenga mfumo wa kujichunguza na kujiwajibisha yenyewe.”
“Serikali imeudhihirishia umma kuwa haikuwa na nia ya dhati ya kuchunguza suala la mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi, bali ilikuwa na lengo la kulisafisha Jeshi la Polisi na kuwalinda maofisa wake.”
Dk Bisimba alisema tangu mwaka 2001 hadi sasa, kituo hicho kimekuwa kikifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali ya mauaji yanayoendelea kufanywa na vyombo vya dola na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika.

Werema ashangaa, mawakili watofautiana
Akizungumzia suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema alisema hana taarifa za Serikali kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya The Hague.
“Kwa nini wameamua kutushtaki katika Mahakama ya The Hague? Kwani hapa nchini hakuna mahakama au wameona ni bora wavuke mipaka... Kwa sasa siwezi kulizungumzia zaidi suala hilo.”
Wakili wa Kujitegemea, Gaudioz Ishengoma alipotakiwa kuzungumzia hilo alisema anaunga mkono uamuzi wa kituo hicho kuipeleka Serikali kwenye Mahakama ya Kimataifa.
Alisema hilo ndilo eneo sahihi ambalo Serikali inatakiwa kupelekwa kwa sababu ya ukiukaji wa haki za binadamu na kwamba huko ndiko ambako haki inaweza kupatikana.
Hata hivyo, Wakili mwingine wa Kujitegemea, Majura Magafu alipinga hatua hiyo akisema kituo hicho kimekosea kuipeleka Serikali The Hague kwa kuwa imekuwa ikichukua hatua za kisheria dhidi ya makosa mbalimbali ya mauaji ambayo yamekuwa yakitokea.
“Kwa mawazo yangu, hawa LHRC wamekosea nadhani wamefanya hivyo kwa masilahi yao binafsi hasa ili kuonyesha kwamba wanafanya kazi,” alisema.
Alisema hata kama Serikali itakuwa imeshindwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wauaji, kituo hicho kilitakiwa kuishtaki Serikali katika mahakama za hapa nchini.
“Hawa sijui wanataka kutupeleka wapi kwa sababu wananchi wengi wa Afrika wakiwemo wa Kenya wamekuwa wakitaka mashtaka yasipelekwe nje ya nchi, hivi kila kitu tunawategemea Wazungu kwa sababu gani hasa?”

Utaratibu wa mashtaka
Kwa mujibu wa Mahakama hiyo, nchi mwanachama au Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndiyo wanaoweza kuelezea hali ya uhalifu ndani ya mipaka ya Mahakama hiyo na maelezo hayo hupelekwa kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC.
Mwendesha mashtaka mkuu atayapitia na kuanza uchunguzi isipokuwa pale tu atakapoona kuwa hakuna haja ya uchunguzi kwa maana ya kuwa kuna ushahidi wa kutosha juu ya uhalifu husika.
Uchunguzi wa mwendesha mashtaka utahusisha taarifa zote na ushahidi unaotakiwa kutathmini uhalifu unaotajwa huku ukizingatia haki zote za anayetuhumiwa.
Katika kipindi chote cha uchunguzi, mwendesha mashtaka atakuwa akitoa taarifa anazopata kwa Baraza la Awali la Mahakama (Pre-Trial Chamber) ambalo litakuwa na wajibu kwa maelekezo ya mwendesha mashtaka mkuu kutoa hati ya kukamatwa kwa wahusika au hati ya kuitwa mahakamani hapo. Mtuhumiwa anapofika mahakamani hapo, husomewa mashtaka yake ambayo yatakuwa msingi wa kesi nzima.
Baada ya kuthibitishwa kwa mashtaka, kesi hiyo itasikilizwa na Baraza la Awali la Mahakama chini ya majaji watatu na kutoa uamuzi wake wa ama kuwaachia au kuwatia hatiani watuhumiwa.
Tayari ICC imeshawapandisha kizimbani wanasiasa maarufu wa Kenya kutokana na kutuhumiwa kuhusika kuchochea vurugu za uchaguzi nchini Kenya mwaka 2008 ambazo zilisababisha vifo vya watu 1,133.
Wanasiasa hao ni Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, Mbunge wa Eldoret Kaskazini, William Ruto, aliyekuwa Mkuu wa utumishi, Francis Muthaura na Mtangazaji wa Redio ya Kass FM, Joshua Sang.
Chanzogazeti la Mwananchi:

BAADHI YA PICHA ALIZOZIWEKA MASANJA KWA FACEBOOK.

MWANDISHI WA HABARI WA SOMALIA AUAWA.

Zilizosomwa zaidi