Monday, October 8, 2012

Mvua kubwa zatarijia kunyesha leo.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema mvua kubwa zilizotangazwa awali zinatarajiwa kuanza leo katika mikoa ya ukanda wa pwani.Mamlaka hiyo imetangaza hali ya hatari katika ukanda huo na kuwataka wananchi kuondoka katika maeneo hatarishi ya mabondeni ambako maji hukutana.

Hivyo wakazi wa Dar es Salaam na kwingineko wamekuwa na hofu na mvua hizo kwa kuzihofia kutokana na kutangazwa mara kwa mara

Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo tayari wameshamisha familia zao ili kukabilina na tatizo hilo

Hata hivyo hadi kufikia majira ya alasiri ya leo mvua hizo kwa mkoa wa Dar es salaam zilikuwa bado hazijaanza rasmi

Kwa taarifa iliyoipata nifahamishe zimebaini kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik ameshajipanga kwa kuweka mikakati kwa kukabiliana na hatari hiyo.

Rwanda yakana mateso na dhulma

Rais wa Rwanda Paul Kagame

Serikali ya Rwanda imepuuza madai kuwa maafisa wake wa usalama waliwatesa na kuwadhulumu watu.
Waziri wa sheria, Tharcisse Karugarama, amesema kuwa madai hayo ambayo yako kwenye ripoti ya shirika la Amnesty International, yalikuwa ni njama ya kutaka kuipaka tope Rwanda. Rwanda imetaja madai hayo kama upuzi mtupu.
Lakini alisema kuwa maafisa wa usalama walikiuka sheria walipochukua hatua wakati wa mashambulizi ya maguruneti katika mji mkuu Kigali miaka miwili iliyopita.
Aliongeza kuwa, washukiwa walizuiliwa kinyume na sheria huku akitaja hatua za maafisa hao wa usalama kama ambazo zilizokuwa na kishindo.
Amnesty International imeitaka Rwanda kuchunguza madai dhidi ya maafisa wake wa ujasusi kuwa waliwazuilia watu kinyume na sheria pamoja na kuwatesa.
Kwa mujibu wa shirika hilo kati ya mwezi Machi mwaka 2010 na mwezi Juni mwaka huu, lilikusanya taarifa za madai ya visa 45 vya kuwazuilia watu kinyume na sheria na vingine kumi na nane vya mateso na dhulma.
Aidha shirika hilo lilikubali kuwa Rwanda inapiga hatua katika kukabiliana na mateso na dhulma lakini serikali imekanusha kuwa ilifanya vitendo kama hivyo.
Washukiwa wengi walikamatwa na kuzuiliwa kufuatia milipuko kadhaa ya maguruneti, mjini Kigali mwezi Machi mwaka 2010 na pia wakati wa kampeini za uchaguzi mwaka huo.
Waziri wa sheria hata hivyo alikiri kuwa huenda maafisa wa usalama waliwazuilia washukiwa kwa muda mrefu kinyume na sheria.
:chanzo BBC

MATOKEO YA MECHI ZA LEO BARANI ULAYA HAYA HAPA.





Liverpool's Luis Suarez


Mkurugenzi mtendaji wa NBC arejeshwa kazini

 TUHUMA za uongozi mbaya, rushwa na wizi zilizotolewa dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru zimefutwa na kiongozi huyo amerejea kazini. 

MWANAFUNZI ALIYEJIFUNGULIA KWENYE MTIHANI ASEMA:

Ufukara umenisababishia mimba : “NILIAMUA kutumia kila mbinu kuficha mimba yangu ili isionekane, kwa sababu ningelifukuzwa shule wakati mimi nilitaka kuhakikisha nafanya mtihani wa darasa la saba ili nifaulu kwenda sekondari, lakini naona Mungu hakupennda. Kutoka Habari leo

MATOKEO YA MCHEZO MJINII BUKOBA, YANGA DHIDI YA KAGERA SUGAR

Matokeo ya mchezo wa leo huko ,
Kaitaba mjini Bukoba Kagera Sugar na Yanga ,Yanga imefungwa goli 1-0 dhidi ya Kagera Sugar ,goli limefungwa na Phemi Felix

KAMA ULIMISI MECHI ZILIZOCHEZWA BARANI ULAYA JANA TAR 7 OCT, MATOKEO YAKO HAPA

Cristiano Ronaldo and Lionel Messi

AS Roma2 - 0Atalanta

Catania2 - 0Parma

Fiorentina1 - 0Bologna

Siena1 - 2Juventus

Torino0 - 1Cagliari

US Pescara0 - 3Lazio

AC Milan0 - 1Internazionale

Napoli

HIZI NDIO STORY KUBWA KATIKA MAGAZETI YA LEO TAR 8 OCT

Zilizosomwa zaidi