Sunday, September 30, 2012


Katika mashambulio ya kulipiza kisasi, kundi la vijana lashambulia Wasomali wa Eastleigh.

Unaikumbuka hii hapa ya jana.


Kiper wa Arsenal Vito Mannone afungwa

Chelsea imekuwa timu ya kwanza kuichapa Arsenal katika mechi za ligi kuu ya Uingereza msimu huu baada ya kuwachapa 1-2 katika uwanja wao wa nyumbani,Emirates siku ya Jumamosi.
Vijana wa Roberto Di Matteo ndio walikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 20 kupitia mshambulizi

Fernando Torres baada ya mkwaju wa adhabu kupigwa na Juan Mata.
Lakini katika dakika ya 42 mshambulizi Gervinho alifunga bao safi hivyo kuzifanya timu hizo mbili ziende mapumzikoni zikiwa sare ya 1-1.
Na katika dakika ya 52 ya kipindi cha pili, Mata alipiga mkwaju mwengine wa adhabu ambapo ulimshinda mlinzi Laurent Koscielny na badala yake kumgonga mguu na kuingia ndani huku ikimuacha Kiper wa Arsenal Vito Mannone hoi.
Wenger amekua akilalamika kwamba safu yake ya nyuma imekuwa ikizembea katika mipira ya adhabu.
Licha ya kufungwa huko, Arsenal walitawala ngoma hiyo nzima ya Jumamosi lakini safu ya mbele ya vijana hao wa Arsene Wenger iliyonekana kukosa makali na kuwa na kukosa umakini.

Mtoto mmoja amekufa na wengine kujeruhiwa kwenye shambulio la guruneti dhidi ya shule ya Jumapili ya watoto wa Kikristo.

Hata bongo kuna mikoko ya kueleweka.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, akiwakabidhi kadi ya uwanachama wa chama hicho kwa Lilian Wassira na ndugu yake Esther, baada kujiunga na chama hicho. Lilian na Esther ni watoto wa George Wassira Kaka wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano) Stephen Wassira. Picha na Michael Matemanga

Zilizosomwa zaidi