Wednesday, September 26, 2012

Okwi kuikosa mechi ya Simba na Yanga. Shirikisho la soka nchini TFF, limethibitisha adhabu ya Emmanuel Okwi ya kuikosa mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa Oct 3. Hii ni baada ya Okwi kupewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu. Afisa habari wa shirikisho hilo Bw Boniface Wambura amesema "Okwi atakosa jumla ya mechi tatu ikiwemo ya oct 3, pia atalipa faini ya laki tano"

Tayari mvua zimeanza kunyesha mkoani mwanza. Baadhi ya wakazi jijini Mwanza wamesema kuwa mwaka huu mvua zimeanza kunyesha mapema na hivyo hawana budi kuanza kuandaa mashamba kwa ajiri ya kupanda mazao.

Vijana wajitokeza uchaguzi CCM. Wakati chama cha mapinduzi kikiendelea na uchaguzi wa chama, vijana wenye umri wa miaka arobaini (40) na wasomi wa elimu ya juu ndio waliojitokeza kuchukua fomu. Akiongea katibu mwenezi wa chama hicho Nape Nnauye, amesema kuwa chama hicho kimepanga kuleta mabadiliko katika utendaji, "Nimeshuhudia kuona asilimia 50 ya waliochukua fomu ni vijana" .

Tume ya kukusanya maoni inapoendelea na mchakato wa kukusanya maoni katika maeneo mbalimbali, tume hiyo imebaini kuwa wanafunzi kuanzia shule za msingi, sekondari na vyuo nchini wamejitokeza na kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni ya uundaji wa katiba mpya.

Baada ya wizara ya usafirishaji kupiga marufuku uchimbaji dawa barabarani, sasa vyo vilivyojengwa katika vituo mbalimbali vyatia aibu kwa uchafu. Miongoni mwa vyoo vinavyoongoza kwa uchafu ni vile vilivyojengwa katika mzani wa msata huko pwani. Hii imeelezwa na baadhi ya wasafiri waliopita katika kituo hicho.

Zilizosomwa zaidi