Friday, September 21, 2012

Kocha wa timu ya Yanga atimuliwa .

Arusha ni soo.

Wafuasi wa Chadema mjini Arusha wakisukuma gari alilokuwa akiendesha aliyeuwa Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema, jana, baada ya kuahirishwa kesi ya kupinga hukumu iliyomvua ubunge wake. Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na wakili wa wajibu rufaa,Alute Mughwai na ndugu yake Tundu Lissu ambaye ni wakili wa waleta maombi kufiwa na baba yao.

Yaliyojili Pakstan kuhusu filamu ya Marekani 

          Maandamano Pakistani
Nchini Pakistan, serikali imetenga siku maalum kwa jina "special day of love" kwa miniajili ya kumsifu Mtume Muhammad.
Marekani imelipia matangazo ya kibiashara nchini Pakistan, rais Obama akionekana kukashifu vikali filamu hiyo
Maandamano makubwa kupinga filamu hiyo tayari yamesababisha vifo sehemu mbali mbali duniani.
Ingawa Marekani ndiyo imeathirika zaidi kutokana na mandamano hayo, uchochezi umeoneka kuongezeka kutoka barani Ulaya baada ya jarida moja nchini Ufaransa kuchapisha picha za kumfanyia mzaha Mtume na waisilamu waliopinga vikali filamu hiyo.
Pakistan imetoa wito kwa watu nchini humo kuandamana kwa amani.
Vyama vyote rasmi vya kisiasa pamoja na mashirika ya kidini wametangaza maandmano kwa ushirikiano na makundi ya kibiashara huku maandamano hayo yakitarajiwa kuwa makubwa sana.
Waziri wa mambo ya nje nchini humo, Hina Rabbani Khar, ameambia shirika la habari la AP kwamba siku hiyo maalum inanuiwa kushinikiza maandamano ya amani na kuzuia watu wenye msimamo mkali kusababisha ghasia kutokana na hasira yao dhidi ya Marekani.
Duru zinasema kuwa vituo vya mafuta, maduka na masoko yatafungwa leo na huenda usafiri ukasitishwa .

Ghasia zaidi mgodini huko Afrika Kusini

Polisi wa Afrika Kusini
Polisi wa Afrika Kusini
Kumekuwa na ghasia zaidi katika mgodi wa Marikana nchini Afrika Kusini ambako polisi wametumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wafanyakazi wa mgodi huo ambao wamekuwa wakiandamana magharibi mwa mji mkuu wa Pretoria.
Polisi hao walivamia makazi ya wafanyakazi hao mapema asubuhi siku ya Jumamosi wakikamata silaha mbalimbali zikiwemo mapanga na mikuki.
Serikali ya Afrika Kusini imeapa kukomesha migomo katika machimbo ya migodi nchini humo.
Migomo hiyo imekuwa ikisambaa na kuendelea tangu polisi walipowaua wachimba migodi 34 katika mgodi wa Marikana hapo Agosti 16 mwaka huu.
Siku ya Ijumaa baraza la mawaziri lilitangaza kuwa halitavumilia kile walichokiita mikutano isiyo halali na kutishia kuwanyanganya silaha waandamanaji hao.
Wanaume kwa wanawake na watoto walitawanyika baada ya polisi waliokuwa wakisaidiwa na helikopta za jeshi zilizokuwa angani zikirusha risasi za mpira na gesi za kutoa machozi kwa waandamanaji.
Maombolezo wakati wa mazishi ya wachimba madini waliouawa
Picha za televisheni zilionyesha watu waliokua na majeraha yaliyochuruzika damu.
"Gari la polisi lilitupita, tulikuwa ni kundi la wanawake na watu wengine walikimbia. Nilisimama pale nikiangalia na walinipiga risasi mguuni," Melita Ramasedi aliliambia shirika la habari la Sapa.
Wakati polisi wakiwasili katika eneo hilo waandamanaji walitumia matairi yaliyowashwa moto kuzuia polisi hao kuingia katika eneo hilo, ripoti zinasema.
Mapema polisi 500 walifanya uvamizi wa makazi ya wafanyakazi hao mapema asubuhi wakikamata silaha mabalimbali, msemaji wa polisi Thulani Ngubane amesema.
Ameliambia shirika la habari la AFP kuwa polisi waliwakamata watu 12 ingawaje watano kati yao ni kwa makosa ya kukutwa na madawa ya kulevya na sio silaha.
"Popote tutakapoana tabia kama hii ya vurugu na watu wakijichukulia sheria mikononi kwa kufanya maandamano yasiyo halali, hakika tutachukua hatua," alisema.
"Polisi hawatasita kuchukua hatua. Tutachukua hatua kama ambavyo tumekwisha anza na tutaendelea kufanya hivyo."
Maandamano hayo yameshuhudia mamia ya wafanyakazi wakiwa na fimbo na mapanga wakipita kutoka mgodi mmoja hadi mwingine eneo la Marikana na maeneo mengine na kutishia yeyote atakayerejea kazini.
a wafanyakazi vimetishia kuitisha mgomo mkubwa.

Hivi ndio vichwa vya habari katika magaazeti ya leo Tar 21 Sep.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Rajabu Rutengwe kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Stalike wilayani Mpanda, jana , baada ya mwenge huo kumaliza kukimbizwa mkoani Rukwa.

Ukiona hali kama hii ujue basi hata elimu ya msingi ina changamoto za kutosha. Hii ni baada ya kutembelea shule moja ya msingi iliyopo katika moja ya kijiji kilichopo katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

Haya ndio mabasi ambayo timu za Simba na Yanga wamepokea kutoka kwa Kampuni ya beer ya Kilimanjaro.

Mamlaka ya dawa Tanzania yabaini dawa bandia za ARVs

MAELFU ya watu walioathirika kwa ugonjwa wa Ukimwi ambao kwa sasa wanaotumia Dawa za Kurefusha Maisha (ARVs) nchini wapo hatarini kufupisha maisha yao baada ya kubainika kuwa toleo mojawapo la dawa hizo la Machi, 2011 ni bandia.

Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kuwa dawa hizo zilizosambaa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mara zilianza kusambazwa tangu Mei mwaka huu na hadi sasa bado zipo sokoni, jambo lililoilazimu Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kuagiza zirudishwe Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

Zilizosomwa zaidi