Thursday, September 20, 2012
Mwanafunzi ajifungua wakati akifanya mtihani wa Hisabati. Huko mkoani kagera hapo jana, mwanafunzi amejifungua mtoto wa kiume alipokuwa akifanya mtihani wa Hisabati ambao ndio ulikuwa wa mwisho katika safari ya elimu ya shule ya msingi. Wazazi na walimu wamesema walikuwa hawajui kama mwanafunzi huyo alikuwa ana ujauzito.
Shule ya sekondari Maranda iliyopo nchini Kenya imefungwa Kwa mda baada ya mabweni mawili kuungua. Tatizo lilosababisha kuungua kwa mabweni hayo bado halijafahamika, wakati huohuo shule ya sekondari ya wasichana iliyopo jirani na Maranda sec. imefungwa kwa tahadhari ya kutokea kwa ajari nyingine kama hiyo.
Wanafunzi wapatao 4,000 wamekosa mkopo kwa mwaka wa masomo 2012/2013 kutokana na ufinyu wa bajeti. Akiongea kaimu Mkurugenzh wa bodi hiyo Bw. Asangye Bangu amesema jumla ya wanafunzi 49,895 walituma maombi kwa bodi ya mikopo, kati yao wanafunzi 33,050 ndio walikidhi vigezo lakini waliopata mkopo ni wanafunzi 29,113. Asilmia 31.9 ni wasichana wakati asilimia 68.0 ni wavulana.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Israel Magesa Wakili Magesa aliyeko (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi. Wakili Magesa, ambaye ni mmiliki wa kampuni y...
-
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu. ...
-
-
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bo...
-
Nimepokea mwaliko wa kikao maalumu cha kikao cha fedha na uongozi wa tarehe 3/01/2014 kikao kufanyika tarehe 06/01/2013 saa nane mchana ...