Wednesday, September 19, 2012

Dar Yanga waendelea kudoda baada ya kukubali kichapo cha goli 3 kwa bila kutoka kwa Mtibwa sugar ya Morogoro, huku Wekundu wa msimbazi wakiendelea kutoa kipigo kwa kuifunga Ruvu JKT goli 2 kwa 0

Wizara ya elimu kweli inachekesha, wanafunzi darasa la saba kujibu mtihani kwa kushedi majibu. Hivi hapa kweli si ndio wale wasiojua kusoma na kuandika watafaulu kuingia kidato cha kwanza.! Hili inabidi kuangaliwa upya na sio kukurupuka tu na mifumo ya ajabuajabu. Hapa ndio wasomi wanaanza kupotea sasa.

Tatizo la vyumba vya madarasa pamoja na madawati limejitokeza tena wakati huu wa mitihani ya darasa la saba. Wanafunzi wa shule ya msingi Ipagala wamejikuta wakienda kufanyia mtihani wao katika shule ya Sekondari Makole baada ya shule yao kukosa vyumba vya madarasa na madawati ya kutosha.

Mradi wa mabasi yaendayo kasi wazinduliwa leo hii na raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo la mradi huu ni kupunguza msongamano na foleni za magari na watu.

Msimamo wa ligi kuu Tanzania leo hii iko hivi: Simba 2-0 Ruvu JKT Mtibwa 3-0 Yanga Toto 2- 2 Azam

Ligi kuu Tanzania bara kuendelea tena katika viwanja tofauti tofauti. Timu zote 14 zinazoshiriki ligi kuu zitakuwa uwanjani leo hii.

Zilizosomwa zaidi