Monday, September 17, 2012
Timu ya watoto wa jangwani Young Afrika wanaendelea na mazoezi yao kuiva mtibwa katika michuano ya ligi kuu Tanzania. Wakati wa mazoezi yao leo hii, kocha wa timu hiyo amesema Kicha walichokipokea Yanga kutoka kwa Prisons ya huko Mbeya jumamosi iliyopita, ilikuwa ni maandalizi mabaya ya timu hiyo. Yanga imeahidi kuonesha tofauti katika michezo ijayo.
Wakazi wa kijiji cha Kwadelo kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodomg walalamika kwa kukosa huduma ya maji. Richa ya kuwa Mkoa huo una asili ya ukame, serikali imewaacha solemba wakazi wa kijiji hicho kwani hata visima havijachimbwa kijijini hapo. Akiongea mkazi wa kijiji hicho ambaye jina lake halikutajwa amesema, inawalazimu wanawake kutembea umbali mrefu usikt wa manane kutafuta maji jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao. Serikali ikishirikiana na wakazi wa Kwadelo imeombwa kulishughulikia tatizo hili mapema kwani wamekuwa wakipata shida hiyo kwa mda mrefu.
Wazazi katika maeneo mbalimbali nchini wameendelea kukemea vitendo vya udanganyifu ambao huwa unajitokeza kwa wanafunzi katika kipindi cha mitihani. Waalimu na wasimamizi watakiwa kuwa makini sana katika kusimamia ili kuepusha swala la wanafunzi kuingia kidato cha kwanza wakati hawajui kusoma na kuandika.
Wakati tukiendelea na wiki ya nenda kwa usalama barabarani, wananchi watakiwa kuwa makini pindi watumiapo barabara ili kupunguza ajari na vifo vitokanavyo na ajari za barabarani. Kwa mkoa wa Dar es salaam ajari za pikipiki zimeripotiwa kuwa nyingi katika kipindi cha August. Wakati huohuo waendesha pikipiki wilayani kasulu mkoani Kigoma wanaendelea kunufaika na wiki hii ya nenda kwa usalama kwani chuo cha mafunzo ya ufundi FDC wilayani humo, kimeanda kozi fupi ya wiki moja ya kujifunza namna kuendesha pikipiki na kupewa cheti maalum kitakachowasaidia wahitimu hao kupata Leseni ya udereva kwa urahisi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Israel Magesa Wakili Magesa aliyeko (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi. Wakili Magesa, ambaye ni mmiliki wa kampuni y...
-
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu. ...
-
-
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bo...
-
Nimepokea mwaliko wa kikao maalumu cha kikao cha fedha na uongozi wa tarehe 3/01/2014 kikao kufanyika tarehe 06/01/2013 saa nane mchana ...