Saturday, September 15, 2012

Hiki nacho kituko, Msikiti ndani ya Kanisa. Ni baada ya dini ya Kiiskam jijini Dar kununua nyumba iliyokuwa ikitazamana na kanisa moja la kilokole na kuamua kujenga msikiti hapo hapo. Nyumba hiyo na kanisa ni karibu tu paa zake zigusane. Kwa story kamili fuatilia hapa.

Wanachama wa Freemason kujulikana. Tanzania ina wanachama hai wa kikundi hicho cha Freemason zaidi ya 600. Katika wanachama hao nchini ni wale watu maarufu sana, lakini katika wanachama hao viongozi wa nyadhifa za juu Serikalini hawamo.

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara kuanza ligi kwa mbwembwe. Ni baada kuicharaza African Lyon kichapo cha goli 3 kwa nunge bila hata kujitetea jijini Dar, wakati huko Mbeya watoto wa jangwani wakubali kuwa wapole dhidi ya timu ya Prisons katika mchezo uliochezwa huko Mbeya.

Maoni ya wadau mbalimbali walipokutana na Tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya haya hapa. Kuweka kipengere cha kupiga marufuku taraka katika ndoa, Kuruhusu matumizi ya bangi kama sigara nyingine, Kuwaendeleza vijana waliomaliza elimu ya msingi na kushindwa kuendelea, Kila raia mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kulipwa kiwango flani cha mshahara.

Tembo akimbilia mjini Morogoro na kujeruhi watu watatu. Miongoni mwa watu waliojeruhiwa na tembo huyo ni Mohammed Nyabange ambaye ni mwandishi wa habari katika kituo cha redio cha Abood fm kilichopo mkoani humo. Hali za mjeruhi hao zinaendelea vizuri.

Kanisa la Sabado mkoani Mara limetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wanafunzi 100 waliounguliwa na shule. Baada ya shule ya sekondari Ikizu iliyopo mkoani humo kuungua, wanafunzi walipoteza vitu vyao. Hivyo Kanisa la Sabato limeamua kuwasaidia vijana hao.

Serikali ya Uingereza imeipongeza Serikari ya Tanzania kwa kuacha demokrasia kukua zaidi nchini, hii ni kutokana na uhuru waliopewa waandishi wa habari kwa kuweza kuripoti mambo mbalimbali yakiwemo matumizi ya pesa za Umma kutoka serikalini.

Alichokisema mwandishi maarufu wa vitabu Ngugi Wathiong'o kutoka nchini Kenya hiki hapa. Sera mbovu ya serikali yetu ndio inayokwamisha maendeleo ya lugha ya Kiswahili katika kukua na kuenea duniani.

Ligi kuu ya Tanzania kuanza kutimka leo jijini Dar. Unadhani mwaka huu nani bingwa??.

Serikali nchini Kenya imepiga marufuku matumizi ya simu feki. Hii ni pamoja na kupiga marufuku uingizaji wa simu feki nchini humo.

Mtoto mmoja asadikiwa kufa katika mto Rwiche uliopo mkoani Kigoma. Imeripotiwa kuwa mtoto huyo huenda ameliwa na Kiboko kwani katika mto huo kuna nyoka hao aina ya kiboko.

Zilizosomwa zaidi