Monday, September 10, 2012

Walimu zaidi ya 300 wamevamia ofisi ya Mkurugenzi huko Lindi kudai pesa zao walizokatwa kutokana na madai ya kushiriki katika mgomo uliofanyika hivi karibuni nchini.

Kumbukumbu za kihistoria leo tar 11 septemba. 1853-Simu ya kutumia umeme ilitumika kwa mara ya kwanza. 1875-Gazeti la kwanza la cartoon liliandikwa. 1885-Moses Hopkins alitajwa kuwa Waziri wa Liberia. 1888-Mwanasiasa mkongwe nchini Algentina Domingo Sarmiento aliuawa. 1895-Kombe la ligi kuu FA, liliibiwa huko Birmingham.

Yondani, Twite kubaki Yanga. Baada ya kika kilichohusha wajumbe wa kamati ya nidhamu kuketi hapo jana jijini Dar, maamuzi ilikuwa ni kuwapeleka wachezaji Yondani na Twite katika club ya watoto wa jangwani Young Sports Club.

Wakati tume ya kukusanya maoni ya uundaji wa katiba mpya, mchungaji Christopher Mtikila UDP, ajiandaa kufungua kesi kupinga mchakato wa katiba. Sababu zinazohusika katika ufunguzi wa kesi hiyo bado hajaziweka hadharani.

Baada ya vuta nikuvute kati ya jeshi la polisi na waandishi wahabari jijini Dar, sasa waandishi wa habari waruhusiwa kufanya maandamano hapo kesho. Kamanda wa polisi Suleiman Kova amethibitisha kuwepo kwa maandamano. Maandamano hayo ni ya kupinga mauaji ya mwandishi Daud Mwangosi yaliyotokea wiki iliyopita huko iringa. Kilele cha maandamano hayo itakuwa katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar.

BREAKING NEWS

Yale maandaaamano yaliyokuwa yaamepangwa kufanywa  na waandishi wa habari,yamepigwa marufuku kwa madai kuw hayakufuata utaratibu.

Usafiri wa treni kwenye majribio


Haya sasa kitu cha tren kama daladala vile imeanza majaribio leo

Chama cha wananchi CUF kimeanzisha mikutano ya hadhara ya mfulurizo. Katika mkutano uliofanywa na cha hicho jana katika viwanja vya jangwani jijini Dar, Dk Ibrahim Lipumba ameishauri serikali kuweka sera itakayowasaidia wakulima wadogowadogo ili kuimarisha uchumi wa nchi na sio vinginevyo. Aliongeza kuwa nchi nyingi duniani kama vile Denmark zimeweza kujiimalisha kiuchumi kwa kuanza kuimarisha uzalishaji wa wakulima wadogowadogo. Kama serikali na wanaharakati wote watashindwa kufanyia kazi mawazo haya, bado nchi itaendelea kuwa na hali ngumu kiuchumi.

Askofu Mkuu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania K.K.K.T Dk Alex Malasusa, amewaachisa kazi wachungaji wawili katika kanisa k.k.k.t ushirika wa Wazohili jijini Dar kwa tuhuma za kukiuka maadilili ya utumishi katika kazi ya Mungu.

Richa ya kuwa mashindano ya riadha yamekamilika na kufungwa hapo jana katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, changamoto mbalimbali zimeweza kujitokeza katika kipindi chote cha mashindano. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa vifaa ambapo iliwalazimu washiri kukimbi bila kuvaa viatu na wanawake kuvaa sketi badala ya bukta za kiriadha. Hii ni kwa jinsi gani serikali na wizara ya michezo kushindwa kuandaa mashindano haya kikamilifu. Ni vizuri kwa mashindano yajayo kuandaliwa vizuri ili kuukuza mchezo huv wa riadha.

Mpango wa kuwarudisha wakimbizi makwao umeanza kugonga mwamba. Hii ni baada ya wakimbizi kutoka nchini Burundi na DRC kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni ya uundaji wa katiba mpya mara baada ya tume ya kukusanya maoni ilipofika katika mkoa mpya wa Katavi.

Zilizosomwa zaidi