Friday, September 7, 2012
WAZO LANGU. Haya makundi mbalimbali vya muziki maarufu kama "Mduara" yanatoa wapi maadili na ujasiri wa watoto wa kike kukata viono hadharani wakiwa wamevalia Khanga moja? Kama ni uhuru basi wasanii Tanzania wamepewa uhuru uliopitiliza hadi kufikia hatua ya wasanii wenyewe kushindwa kujiheshimu. Hivi kizazi cha leo watoto wanajifunza nini kupitia mchezo kama huo? Ni vizuri basi wasanii walioachiwa huru kuhusika katika muziki huo kufuata maadili, kwani kushindwa kwao kufuata maadili kinachofuata ni kujiabisha wenyewe na taifa kwa ujumla. Pia serikali iliangalie suala hili kwa jicho la pili ili kulinusuru taifa katika wimbi hili zito la "Khanga moja ndembendembe".
Zaidi ya waumini 300 wa dini ya Kiislam wameandamana jijini Dar es salaam. Maandamano ya waumini hao ni kuitaka serikali kuwaachia huru waislamu wote waliokamatwa kwa madai ya kupinga shughuli ya Sensa. Kutokana na kuandamana kwao, tayari serikali imetoa tamko la kuwaachia huru wote waliokuwa wakishikiliwa na jeshi la polisi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Israel Magesa Wakili Magesa aliyeko (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi. Wakili Magesa, ambaye ni mmiliki wa kampuni y...
-
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu. ...
-
-
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bo...
-
Nimepokea mwaliko wa kikao maalumu cha kikao cha fedha na uongozi wa tarehe 3/01/2014 kikao kufanyika tarehe 06/01/2013 saa nane mchana ...