Monday, August 27, 2012
Diamond Plutnum kufanya kolabo na J Martin. Hii ni baada ya kufanya shoo kali katika mashindano ya Big Brother Africa na hivyo kuanza kualikwa sehemu mbalimbali kutoa burudani. Hivi sasa Diamond amesema tayari ameshaingiza voko za wimbo huo kwa producer Marco Chali na sasa amesubiri kuingiza voko za J Martin ambaye hivi sasa yupo nchini Marekani
Nape aigomea Chadema. Baada ya mbunge wa Ubungo, John Mnyika kutoa siku saba kabla ya kwenda mahakamani,kuitaka CCM kuilipa Chadema fidia ya Sh. Bilion 3 kutokana na tuhuma zilizotolewa kuwa Chadema hicho kinapokea mabilioni kutoka nje, Katibu mwenezi wa CCM, Nape Nnauye amewaeleza waandishi wa habari kuwa chama hakotayari kulipa fidia yoyote, "kama ni kwenda mahakamani waende hata kesho wasisubiri siku saba kwani watapoteza mda" pia amemtaka katibu wa Chadema, Wilbrod Slaa kutoa uthibitisho kwa madai aliyoyatoa kuwa CCM inaingiza siraha nchini. Kwa upande wa kulipwa fidia, Nape ameitaka Chadema kuilipa CCM Sh. Bilion 3.1
Kituko kimetokea mkoani Tabora baada ya ziara ya kushtukiza iliyofanywa na mkuu wa mkoa katika stendi ya mabasi ya mkoa huo. Katika usiku wa kuamkia siku ya Sensa mkuu wa mkoa huo Bi Fatuma Mwasa aliitembelea stendi hiyo na kuikuta ina uchafu usioelezeka jambo lililomfanya bi Fatuma kuwakurupusha Watendaji wa wilaya ya Tabora mjini usiku huo kufika na kuanza kufanya usafi mara moja, muda huohuo. Kwa aibu waliyoipata watendaji hao, waliamua kuwapa tenda vijana wakafanya usafi ndani ya stendi usiku huo.
Timu ya mpira wa miguu Azam, imemtimua rarmi kiungo kutoka Kenya George Odhiambo 'BLACKBERY' kutokana na utovu wa nidhamu katika timu hiyo. Msemaji wa timu hiyo amesema Odhiambo hakufika mazoezini takribani siku nne bila kutoa taarifa. Aliongeza kuwa nafasi yake itachukuliwa na mchezaji mwingine mapema iwezekanavyo.
Waislam mkoani Kigoma katika maeneo ya Mwandiga nje Kidogo ya mji wa Kigoma, wameisusia shughuli ya sensa na kugoma kuhesabiwa kwa kuamua kukaa msikini. Kitendo hiki kimefanywa na baadhi ya Masheh katika msikiti wa Mwandiga kuwahamasisha waislam kwenda kukaa msikitini. Walipotaka kuhojiwa, walikataa, na hawakuongea lolote.
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu yakabiliwa na tuhuma za Ubadhilifu wa pesa. Imeripotiwa kuwa vigogo katika bodi hiyo hujilipa mishahara minono, kigogo mwingine aajiri ndugu zake 11 wasio na sifa. Mpaka sasa pesa iliyokusanywa na Bodi hiyo ni bilion 9 tu, na zaidi ya bilion 300 hazijakusanywa bado. Chanzo: Jamii forum
Subscribe to:
Posts (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Israel Magesa Wakili Magesa aliyeko (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi. Wakili Magesa, ambaye ni mmiliki wa kampuni y...
-
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu. ...
-
-
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bo...
-
Nimepokea mwaliko wa kikao maalumu cha kikao cha fedha na uongozi wa tarehe 3/01/2014 kikao kufanyika tarehe 06/01/2013 saa nane mchana ...