Thursday, August 16, 2012

Kama una sherehe ya ndoa, send off, birthday au mahafari na unahitaji kupata MC na Dj mzuri, wasiliana nasi

"Kama mwanahalisi hawakuridhika na adhabu waliyopewa, wakate rufaa" Hiyo ni kauri ya waziri mkuu Mizengo Pinda alipokuwa akieunga vikao vya Bunge ambavyo vitaanza tena octoba.

Dk Ulimboka awaambia Watanzania wasiwe na wasiwasi juu yake, "siku inakuja ambapo nitaweka mambo yote hadharani" Kauli hii ameitoa hapo jana alipokuwa akiongea na wandishi wa habari jijini Dar kwani maswali mengi yalihusu lini atawaweka bayana Watanzania.

Slaa, Nape uso kwa uso. Dk Slaa (chadema) aamua kumfungukia Nape (Ccm) baada ya Nape kuwatuhumu chadema kwa kutumia pesa za harambee badala yake Slaa amemtaka Nape kuwaeleza wanachama wake jinsi gani CCM ilivyotumia pesa chafu katika uchaguzi wa mwaka 2005 na kuingia madarakani.

Kwa mashabiki wa Koffi Olomide hii inawahusu. Baada ya kutumia nguvu na kumrushia ngumi meneja wake Diego Lubasu akidai pesa, sasa afungwa jela miezi mitatu. Koffi alikamatwa na polisi hapo jana ambapo alifikishwa mahakani na kuhukumiwa adhabu hiyo.

Kama una sherehe za ndo, birthday, na mahafari na unataka kupata MC na Dj mzuri, wasiliana nasi.

Dk Steven Ulimboka aanza kuongea baadhi ya mambo tangu alipowasili nchini kutoka Afrika kusini kwa matibabu baada ya kupigwa vikali. Amesema yeye pekee ndio anayeujua mtandao wote katika mkasa wa kupigwa kwake. Amesisitiza kuwa "hakuna yeyote anayejua kuhusu hili"

Rais wa Malawi Joyce Banda amesema hayuko tayari kupigana vita ya kijeshi. Amesema hawezi kupigana na majirani zake wa karibu kabisa watanzania eti kwa sababu ya ziwa Nyasa.

Wakati waziri mkuu Mizengo Peter Pinda akiahirisha vikao vya bunge, amewataka watanzania wote kushiriki kikamilifu katika shughuli ya sensa na kuwataka kushirikiana vyema na makarani wa sensa.

Kama una sherehe na unahitaji Mc, wasiliana nasi.

Van Persie kutua Man U. Baada ya kiungo huyo kutwaliwa kutoka Arsenal, sasa Man U yamtegemea sana Van Persie katika kulitwaa kombe ya ligi kuu ya Primear.

Zilizosomwa zaidi