Sunday, August 12, 2012

Tanzania imedoda katika mashindano ya Olympic. Hapo jana mashindano ya olympiki yamefikia tamati wakati wawakilishi wote kutoka Tanzania bila kunyakua medali katika mchezo wowote.

Kuchangia maoni katika kuunda katiba mpya ni jukumu la kila mtanzania. Shiriki kikamilifu uone thamani ya mchango wako.

Wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambao wamekwishakamilisha malipo ya kuunganishiwa umeme na shirika la Tanesco wilayani wametakiwa kufuatilia huduma hiyo mapema sana. Hayo yamesemwa na naibu Waziri wa nishati na madini Bw Masele alipofanya ziara katika mkoani Kigoma.

Wabunge wataka vikao vinapoendeshwa visioneshwe kwa wananchi moja kwa moja. Spika wa bunge Anne Makinda amethibitisha hayo baada ya baadhi wabunge kutaka kuandaa hoja hiyo na kuipeleka bungeni.

Nape awawashia moto Chadema, Hii ni kutokana na harambee zinazofanywa na Chadema katika kipindi hiki cha vuguvugu la mabadiliko.

Dk Steven Ulimboka arejea nchini kutoka Afrika Kusini alipokuwa akipewa matibabu. Baada ya kupigwa vibaya na watu wasiojulikana hali yake ilikuwa mbaya sana hadi kufikia hatua ya kupelekwa Afrika kusini kwa matibabu. Hadi hivi sasa hali yake inaendelea vizuri.

Kampuni ya simu za mkononi Vodacom, imeleta vocha mpya yenye thamani ya shilingi 450, zile za shilingi 500 zinatoweka. Hii inakaa vipi kwa kampuni ya Vodacom Tanzania

Mgogoro wa mpaka unaoendelea kati ya Tanzania na Malawi, umewafanya Wamalawi kujaa katika ubarozi Dar

Godbless Lema amtaka Dr Wilibrod Slaa kugombea ubunge Arusha mjini.

Naibu waziri wa vijana nchini Costa Rica Bi Karina Bolanos, amefukuzwa kazi baada ya kuoneshwa kwa mkanda wa ngono.

Zilizosomwa zaidi